Maelfu ya waandamanaji wanaounga mkono Palestina wamekusanyika katika Uwanja wa Beyazit Istanbul siku ya Jumamosi baada ya swala ya alasiri kupinga mauaji ya halaiki yanayoendelea kufanywa na Israel na kusababisha njaa ya lazima Gaza.
Maandamano hayo, ambayo pia yameshirikisha mashirika yasiyo ya kiserikali na wananchi, yalielekea katika msikiti wa kihistoria wa Ayasofya.
Washiriki wametaka kupaza sauti ya janga la kibinadamu na kuonyesha mshikamano na watu wa Gaza huku mashambulizi yakiendelea na uhaba wa chakula na dawa.
Waandaaji wameitaka jumuia ya kimataifa kuchukua hatua za haraka kumaliza mateso yanayoendelea.
Israel inalaumiwa kwa mauaji yake ya halaiki Gaza, ambapo imeua zaidi ya watu 61,000 tangu Oktoba 2023.
Kampeni ya kijeshi imelisambaratisha eneo hilo na kusababisha vifo vitokanavyo na njaa.
Novemba mwaka jana, Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa ilitoa hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu pamoja na aliyekuwa Waziri wake wa Ulinzi Youv Gallant kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu Gaza.
Israel pia inakabiliwa na kesi ya mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Haki ya Kimataifa kwa vita vyake katika eneo lilizingirwa.