UTURUKI
2 dk kusoma
Uturuki na Senegal wadhamiria kuendeleza urafiki chanya ushindi wa pande zote
Miradi inayoendelea ya ujenzi, nishati, madini, chakula na sekta ya ulinzi inaimarisha zaidi uhusiano kati ya Uturuki na Senegal - Waziri wa Biashara wa Uturuki Prof. Dk. Ömer Bolat.
Uturuki na Senegal wadhamiria kuendeleza urafiki chanya ushindi wa pande zote
Jukwaa la biashara la Uturuki- Senegal lilijadili Hatua za kuimarisha mfumo wa kibiashara na kisheria, hasa Mkataba wa Kuepuka Ushuru Mara Mbili. / TRT Afrika Swahili
9 Agosti 2025

Uturuki na Senegal wamejadili lengo la pamoja la kuongeza kiwango cha biashara baina ya nchi hizo mbili hadi dola bilioni 1 katika muda wa kati, kulingana na lengo lililowekwa na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan.

Katika mkutano baina ya Waziri wa Biashara wa Uturuki Prof. Dk. Ömer Bolat na Waziri Mkuu wa Senegal Ousmane Sonko uliofanyika sambamba na Jukwaa la Biashara la Uturuki-Senegal Waziri Dkt Bolat alisifia fursa mpya za ushirikiano katika uwekezaji, kandarasi, tasnia ya ulinzi, nishati mbadala, na biashara zinazoshika kasi kati ya nchi hizo mbili.

‘‘Miradi inayoendelea ya ujenzi, nishati, madini, chakula na sekta ya ulinzi inaimarisha zaidi uhusiano wetu wa urafiki na udugu,’’ alisema Dkt Bolat.

Wawili hao pia walijadiliana hatua za kuimarisha mfumo wa kibiashara na kisheria, hasa mkataba wa kuepuka ushuru mara mbili.

Upeo wa nchi zote mbili

Waziri Bolat pia alisisitiza fursa za kimkakati zinazotolewa na Senegal aliyoitaja kuwa nyota inayong'aa ya Afrika kwa jumuiya ya wafanyabiashara wa Kituruki.

‘‘Tumedhamiria kuendeleza urafiki wetu uliokita mizizi na Senegal katika siku zijazo kupitia biashara ya pande zote na uwekezaji ndani ya mfumo wa kanuni ya kushinda,’’ aliongeza Bolat.

Kongamano la Biashara na Kiuchumi la Uturuki–Afrika lililofanyika mwaka huu tarehe 16–17 Oktoba mjini Istanbul, chini ya uangalizi wa Rais Erdogan, ulishirikisha nchi 54, huku ukieleka ushirikiano wa kiuchumi kati ya Uturuki na Afrika kwenye upeo mpya.

‘‘Mungu akipenda, baraka za udugu wetu zitaangaza upeo wa nchi zote mbili na kufungua njia kwa ajili ya mafanikio mengi mazuri.’’ alisema Waziri Bolat.

CHANZO:trt
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us