ULIMWENGU
2 DK KUSOMA
Majeshi ya Israeli yauwa Wapalestina 17 na kuharibu mazao
Mashambulizi ya Israeli katika eneo la Gaza yameingia siku ya 267 yakiwa yameuwa Wapalestina takribani 37,834, wengi wakiwa ni wanawake na watoto na kujeruhi 86,858, huku zaidi ya watu 10,000 wakihofiwa kufunikwa na vifusi vya nyumba zilizobomoka.
Majeshi ya Israeli yauwa Wapalestina 17 na kuharibu mazao
Kulingana na mashuhuda, mabomu hayo yalilenga vikundi vya raia, waandishi wa habari na mahema ya watu wasio na makazi./Picha: Reuters              / Others
29 Juni 2024

Takribani Wapalestina 17, wakiwemo waandishi wa habari, wameuwawa na majeshi ya Israeli katika maeneo tofauti ya eneo la Gaza.

Timu za madaktari zililiambia shirika la habari la Anadolu kuwa Wapalestina 13 waliuwawa kufuatia shambulio la bomu katika eneo la al-Shakoush, lililoko kaskazini mwa Rafah, kusini mwa Gaza.

Kulingana na mashuhuda, mashambulizi hayo yaliwalenga waandishi wa habari, raia wa kawaida wa watu waliokosa makazi.

Duru za kiafya pia zimesema kuwa Wapalestina wanne waliuwawa na wengine 10 kujeruhiwa katika shambulio la bomu lililolenga makazi ya familia ya Al Ghazi katika kitongoji cha Sabra, kusini kwa mji wa Gaza.

Wakati huo huo, mashuhuda wanasema kuwa vifaru na matingatinga ya kijeshi yaliharibu eka 1,235 za mazao ya mbogamboga, kaskazini mwa Rafah, eneo pekee lililotengwa kwa shughuli hiyo.

pata habari zaidi kupitia whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us