UTURUKI
2 dk kusoma
Uturuki kuanza kutengeneza vifaru vya kivita vya 'Altay' kwa wingi
Kiwanda hicho cha Ankara kitatengeneza vifaru vya kisasa na magari ya kivita ya kujihami, ikiwa hatua kubwa katika mradi wa Uturuki wa kuwa na uwezo wa ulinzi na kujihami.
Uturuki kuanza kutengeneza vifaru vya kivita vya 'Altay' kwa wingi
Kikiwa na teknolojia ya kisasa, kifaru cha Altay kinawezeshwa na injini ya BATU. / AA
tokea masaa 8

Uturuki imeanza rasmi kutengeneza kifaru chake cha kivita cha “Altay,” katika kiwanda chake cha Ankara cha BMC, ikiwa ni hatua kubwa katika mipango yake ya kuimarisha ulinzi wa nchi.

Fuat Tosyali, Mwenyekiti wa BMC, amesema siku ya Ijumaa kuwa mradi huo unatimiza ndoto ya karne ya Uturuki. 

“Kiwanda chetu kimeanza kutengeneza kwa wingi, baada ya kuweka msingi wake mwaka jana — tunatarajia kufikia mahitaji ya Jeshi la Uturuki na washirika wake katika sekta ya ulinzi,” alisema.

Kikiwa na teknolojia ya kisasa, kifaru cha Altay kinawezeshwa na injini ya BATU, iliyotengenezwa ndani ya nchi na BMC Power, kampuni iliyo sehemu ya BMC. 

Kiwanda hicho cha Ankara kinatumia mfumo wa roboti na teknolojia ya kisasa katika kila hatua ya uzalishaji, kuanzia hatua ya mwanzo hadi kukamilika kwake.

‘Hakuna changamoto zozote’

Tosyali alieleza kuwa kampuni ya BATU power, ambayo ina uwezo wa horsepower kuanzia 400 hadi 1,500, inabidi ifanyiwe majaribio kabla kuanza kutumika rasmi. 

“Kampuni ya power inahitaji ‘kufanya kazi’ ya kilomita 10,000 na ifanyiwe tathmini ya utendakazi wake. Kufikia sasa, hakuna changamoto zilizoonekana, na mifumo yote, ikiwemo ya anga na ulinzi, yanafanyiwa majaribio pamoja na kifaru,” aliongeza.

Pamoja na Altay, kiwanda hicho cha BMC kitatengeneza magari ya kisasa ya kivita ya Altug yanayojulikana kama ‘‘eight-by-eight armoured combat vehicle’’.

Rais wa Shirika la Uturuki la Sekta ya Ulinzi (SSB) Haluk Gorgun amepongeza ushirikiano katika mradi huo na kuthibitisha kuwa Rais Recep Tayyip Erdogan amekuwa akifuatilia kwa karibu maendeleo hayo. 

“Vifaru hivyo tulivyovitoa mwaka jana kwa ajili ya majaribio vilionesha uwezo wake wote na kuidhinishwa. Kwa kuwa sasa kiwanda chetu kimekamilika, tutatengeneza na kukabidhi moja kwa moja kwa wanajeshi wetu,” Gorgun alisema.

CHANZO:TRT World and Agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us