UTURUKI
2 dk kusoma
Uturuki yakataa ripoti za vyombo vya habari vya Israel zinazoihusisha na njama ya mauaji
Ankara inasema kutajwa kwa jina lake katika madai ya njama dhidi ya waziri wa Israel ni sehemu ya kampeni ya upotoshaji inayolenga sera yake kuhusu Palestina.
Uturuki yakataa ripoti za vyombo vya habari vya Israel zinazoihusisha na njama ya mauaji
Ankara inasema kutajwa kwa Uturuki katika madai ya njama dhidi ya waziri wa Israel ni sehemu ya kampeni ya upotoshaji inayolenga sera yake. / / AA
tokea masaa 9

Kituo cha Uturuki cha Kupambana na Upotoshaji wa Taarifa kimekanusha ripoti za vyombo vya habari vya Israel zilizotaja Uturuki na kuihusisha na madai ya njama ya kumuua waziri wa Israel, vikieleza kuwa ni sehemu ya kampeni ya makusudi ya kuichafua.

“Kutajwa kwa jina la nchi yetu katika ripoti za baadhi ya vyombo vya habari vya Israel kuhusu madai ya njama ya kumuua waziri wa Israel ni matokeo ya kampeni ya upotoshaji wa makusudi inayolenga Uturuki,” kituo hicho kilisema.

Kituo hicho kilisisitiza kuwa kesi hiyo, ambayo vyombo vya habari vya Israel vimewasilisha kama tukio jipya, kwa hakika inahusiana na tukio lililotokea miezi minane iliyopita.

“Zaidi ya hayo, taarifa za watu waliokamatwa kuthibitisha kuwa hawana uhusiano wowote na Uturuki zimethibitishwa na maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu,” kiliongeza kituo hicho.

Kiliendelea kueleza kuwa lengo kuu la ripoti hizo ni kuunda taswira potofu kuhusu Uturuki katika medani ya kimataifa na kudhoofisha msimamo wake kuhusu Palestina.

“Lengo kuu la habari hizi ni kuunda taswira potofu na ya makusudi dhidi ya Uturuki katika medani ya kimataifa, na hivyo kudhoofisha sera ya Uturuki kuhusu Palestina,” taarifa hiyo ilisema.

Ankara ilitoa wito kwa umma na mamlaka za kimataifa kutopatia uzito juhudi hizo, ambazo ilizieleza kama “upotoshaji na propaganda chafu zinazoilenga Uturuki.”

Uturuki imekuwa miongoni mwa wakosoaji wakubwa wa Israel tangu kuanza kwa mauaji ya halaiki huko Gaza, mara kwa mara ikiishutumu Tel Aviv kwa kutenda mauaji ya halaiki na kutaka iwajibishwe katika mahakama za kimataifa.

Maafisa wa Ankara wanasema kampeni za kuichafua Uturukiu kwa kuuhusisha na ugaidi au njama za kikanda ni sehemu ya njama za kudhoofisha msimamo wake wa kidiplomasia wa kuiunga mkono Palestina.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us