AFRIKA
1 dk kusoma
Ripoti: Ofisi ya Rais Ruto yatumia zaidi ya dola elfu 15 kwa huduma za uchapishaji kwa siku
Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kenya imetumia zaidi ya dola elfu 15 sawa na shilingi milioni 2 za Kenya kwa siku katika huduma za uchapishaji katika mwaka uliopita wa kifedha.
Ripoti: Ofisi ya Rais Ruto yatumia zaidi ya dola elfu 15 kwa huduma za uchapishaji kwa siku
Bajeti ya uchapishaji iliongezeka kutokana na idadi kubwa ya wageni waliokuwa wakialikwa Ikulu kushiriki mkutano wa Rais. / / Reuters
3 Septemba 2025

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msimamizi wa Bajeti, Bi Margaret Nyakang’o.

Ripoti hiyo, ambayo imebainisha matumizi ya kupindukia na yasiyo ya lazima serikalini, imeonyesha pia kuwa ofisi ya Rais William Ruto ilitumia zaidi ya dola milioni 7 sawa na shilingi bilioni 1 za Kenya kwa ajili ya malipo ya washauri wake, ambao sasa wamefikia 20 chini ya utawala wa Kenya Kwanza.

Licha ya ahadi zilizotolewa za kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ili kuziba pengo la bajeti, ripoti inaonyesha kuwa serikali haina utashi huo.

Huduma hizo za uchapishaji zilihusisha matumizi ya karatasi kwa ajili ya kuchapisha sera za serikali, maagizo ya Rais, matangazo rasmi yaliyotumwa kwa mashirika ya serikali, mikataba ya utendaji, taarifa kwa vyombo vya habari kila baada ya wiki mbili, mawasiliano ya mara kwa mara ya serikali nyakati za dharura, pamoja na huduma nyengine.

Aidha, bajeti ya uchapishaji iliongezeka kutokana na idadi kubwa ya wageni waliokuwa wakialikwa Ikulu kushiriki mikutano na Rais, hali iliyohitaji uchapishaji wa kadi za mialiko kwa kutumia karatasi za ubora wa juu.

Ripoti hii inakuwa wakati ambapo, serikali ya nchi hiyo, iko mbioni katika kunadi sera ya matumizi rafiki ya mazingira ikiwemo kupunguza matumizi ya karatasi.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us