AFRIKA
2 dk kusoma
Mwanamfalme wa Qatar ataka kuwekeza dola bilioni 21 DRC,serikali ya nchi hiyo imesema
Mwanamfalme wa Qatar Sheikh Mansour bin Jabr bin Jassim Al Thani anataka kuwekeza dola bilioni 21 nchini DRC, serikali ya nchi hiyo ilitangaza siku ya Jumatano.
Mwanamfalme wa Qatar ataka kuwekeza dola bilioni 21 DRC,serikali ya nchi hiyo imesema
Mwanamfalme wa Qatar Sheikh Mansour bin Jabr bin Jassim Al Thani ana mpango wa kuwekeza mabilioni ya madola nchini DRC. / TRT Afrika English
tokea masaa 16

Shirika la uwekezaji la Al Mansour Holding linatarajia kuwekeza dola bilioni 21 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo Qatar ni mpatanishi kwa lengo la kumaliza vita vya miaka mingi mashariki mwa nchi, serikali ya DRC ilitangaza siku ya Jumatano.

Mwanzilishi wa shirika hili na mmoja wa Wanamfalme Sheikh Mansour bin Jabr bin Jassim Al Thani alifanya ziara mji mkuu wa DRC, Kinshasa siku ya Jumanne ikiwa sehemu ya ziara yake ya bara la Afrika.

Ujumbe wa Qatar uliwasilisha ‘‘mapendekezo" ya kutaka kuwekeza karibu dola bilioni 21 nchini DRC wakati wa mkutano na Waziri Mkuu Judith Suminwa, ofisi yake ilisema katika taarifa.

Uwekezaji huo utakuwa katika sekta mbalimbali, ikiwemo kilimo, fedha, uchimbaji madini, dawa na haidrokaboni, iliongeza.

Kufanya ziara 'ya kibinafsi' DRC

Shirika la habari la AFP, lilipowasiliana nao, Afisa mmoja wa Qatar alisema Sheikh Mansour alikuwa anafanya ziara ya kibinafsi DRC kama mfanyabiashara.

Mapigano katika eneo la mashariki mwa DRC kwenye utajiri mkubwa wa madini yameongezeka mapema mwaka huu baada ya waasi wa M23 kuanzisha mashambulizi, na kufanikiwa kudhibiti miji mikuu miwili ya mkoa katika kipindi cha wiki chache.

Juhudi za kidiplomasia kutafuta kumaliza mzozo huo zilikwama hadi ghafla Qatar ilipotangaza kuwa Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi walikutana jijini Doha kwa mazungumzo katikati ya mwezi Machi.

Nchi hizo mbili zilitia saini makubaliano ya amani mwezi Juni jijini Washington.

Kwa upande mwingine, serikali ya DRC na M23 walianza mazungumzo Doha, mwezi Aprili, na kutangaza kusitisha vita mwezi Julai. Hata hivyo, mapigano yameendelea katika eneo hilo.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us