AFRIKA
1 dk kusoma
Jumuiya ya Nchi za Kiarabu yaifutia Somalia deni la miaka 38
Somalia imeishkuru Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, ikieleza uamuzi huo kuwa mafanikio ya ''kihistoria''.
Jumuiya ya Nchi za Kiarabu yaifutia Somalia deni la miaka 38
Deni la ada ya uanachama wa Somalia katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ni malimbikizo ya zaidi ya miaka 38
tokea masaa 12

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imeifutia deni la asilimia 75 Somalia kwa kile Balozi wa Somalia nchini Misri na Mwakilishi katika Jumuiya hiyo, Ali Abdi Aware, ameeleza kuwa mafanikio ya ‘‘kihistoria’’.

Balozi Aware alihutubia mkutano wa 164 wa Wawakilishi katika Jumuiya hiyo siku ya Jumanne mjini Cairo.

Alitoa shukrani za Somalia kwa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na wanachama wake kwa kuunga mkono Somalia kuomba kufutiwa deni ambalo limekuwepo kwa miaka 38 lililotokana na kutolipa ada ya uanachama.

Jumuiya hiyo iliidhinisja kufutwa kwa asilimia 75 ya malimbikizo ya deni, Shirika la Habari la Somalia, Somali National News Agency limeripoti.

Haikufahamika mara moja ni kiasi gani ambacho Somalia ilikuwa inadaiwa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.

Hata hivyo, Aware alisisitiza kuwa kufutiwa kwa deni hilo ni kutokana na ‘‘juhudi za kidiplomasia’’ za Ubalozi wa Somalia mjini Cairo, ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya uongozi wa taifa la Somalia.

Somalia ilijiunga na Jumuiya hiyo ya Nchi za Kiarabu 1974, miaka kumi na nne baada ya kupata uhuru wake.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us