AFRIKA
1 dk kusoma
Wito wa msaada watolewa baada ya maporomoko ya ardhi kuangamiza kijiji cha Sudan, na kuua watu 1,000
Kundi la watu wenye silaha linloadhibiti sehemu ya magharibi mwa Sudan liliomba msaada wa kigeni Jumanne katika kukusanya miili na kuwaokoa raia kutokana na mvua kubwa, huku kukiwa takriban watu 1,000 walifariki kutokana na maporomoko ya ardhi.
Wito wa msaada watolewa baada ya maporomoko ya ardhi kuangamiza kijiji cha Sudan, na kuua watu 1,000
Serikali ya Sudan ilitoa salamu za rambirambi na kusema iko tayari kusaidia./ / Reuters
3 Septemba 2025

Ni mtu mmoja pekee aliyenusurika na janga hilo katika kijiji cha Tarseen katika eneo la milima la Jebel Marra katika eneo la Darfur, lilisema kundi la ‘Sudan Liberation Movement/A (SLM/A).

SLM/A, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikidhibiti na kutawala sehemu iya Jebel Marra, ilitoa wito kwa Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa ya misaada kusaidia kukusanya miili ya walioathiriwa, ikiwa ni pamoja na miili ya wanaume, wanawake na watoto.

"Tarseen, maarufu kwa uzalishaji wake wa machungwa, sasa imeharibiwa kabisa," kikundi hicho kilisema katika taarifa.

Mvua zinazoendelea kunyesha zimefanya safari katika eneo hilo kuwa ngumu na inaweza kukwamisha juhudi zozote za uokoaji au msaada.

"Wanavijiji jirani wamejawa na hofu kwamba huenda hali kama hiyo itawapata ikiwa mvua kubwa itaendelea kunyesha, jambo ambalo linasisitiza hitaji la dharura la mpango wa kina wa uokoaji na utoaji wa makazi ya dharura," kiongozi wa kundi hilo, Abdelwahid Mohamed Nur aliongeza.

Taarifa ya mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa imeweka idadi ya waliofariki kuwa kati ya 300 na 1,000, ikinukuu ripoti za ndani.

CHANZO:Reuters
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us