AFRIKA
1 dk kusoma
Luhaga Mpina: Sirudi CCM ng’o
Mwanasiasa huyo, ambaye uteuzi wake wa kugombea Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo ulitenguliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo (INEC), amesema kuwa hana nia ya kurejea kwenye chama chake cha CCM.
Luhaga Mpina: Sirudi CCM ng’o
Luhaga Mpina./Picha: Wengine / Others
tokea masaa 8

Aliyekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo cha nchini Tanzania, Luhaga Mpina amesema hana mpango wowote wa kurejea kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza Septemba 3, jijini Dar es Salaam, Mpina ambaye uteuzi wake wa kugombea Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo ulitenguliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo (INEC), amesema kuwa hana mpango wa kurudi ‘nyumbani’, licha ya ombi lililotolewa na mgombea Urais wa CCM, Emmanuel Nchimbi.

“Nimesikia wakizungumza kule jimboni kwangu, oooh, Mpina rudi CCM, nyumba ipi…nishasema sitorudi CCM, nimeondoka CCM, sitorudi CCM,” alisema mwanasiasa huyo na mbunge wa zamani wa jimbo la Kisesa.

Kauli ya Mpina inakuja siku moha baada ya Dkt. Nchimbi kumuomba kurejea kwenye chama chake cha awali CCM.

Akizungumza mkoani Simiyu, Dkt. Nchimbi aliahidi kumpokea Mpina kwa mikono yake miwili, endapo ataamua kurejea CCM.

Akiwa kwenye mchakato wa kuzisaka kura kwenye jimbo la Kisesa, mkoani Simiyu, Nchimbi amesema Mpina hana budi kurudi nyumbani CCM kwa kuwa bado ni sehemu ya familia hiyo ya kisiasa.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us