AFRIKA
2 dk kusoma
Ethiopia yawania kuandaa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu tabianchi 2027
Ethiopia inawania kuwa mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi 2027 katika mji mkuu Addis Ababa, wakiwa kwenye ushindani na Nigeria.
Ethiopia yawania kuandaa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu tabianchi 2027
Ethiopia inawania kuwa mwenyeji wa mkutano wa tabianchi 2027, ikipambana katika hilo dhidi ya Nigeria. / Wengine
tokea masaa 17

Ethiopia imewasilisha ombi la kuwa mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi 2027 katika mji mkuu Addis Ababa, ikiwa katika ushindani huo na Nigeria, ambayo inataka mji wa Lagos uwe mwenyeji.

Karibu nchi 200 hukusanyika kila mwaka kwa wiki mbili "kwa ajili ya kongamano" – linalofahamika kama COP - ambapo majadiliano kati ya serikali kuhusu kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi hufanyika.

"Tuna uwezo, tuna miundombinu, tuna eneo, tayari kwa kuandaa mkutano huo wa tabianchi," Rais wa Ethiopia Taye Atske Selassie aliuambia mkutano wa Umoja wa Mataifa jijini Addis Ababa siku ya Jumatano.

Makongamano ya COP huwa yanazunguka katika maeneo mbalimbali duniani. Nchi 54 ambazo ni wanachama wa Afrika kwa Umoja wa Mataifa zinatakiwa zikubaliane kwa pamoja nani atakuwa mwenyeji wa COP32 mwaka 2027.

Jukumu muhimu katika kuelekeza majadiliano ya masuala ya tabianchi

Kuwa mwenyeji wa kongamano la COP kunatoa nafasi kwa nchi kuwa na jukumu muhimu la kuelekeza majadiliano na fursa ya kuwasilisha vipaumbele vyake.

Kwa muda mrefu nchi za Afrika zimetaka mikutano ya COP iwe na makubaliano ya fedha ili ziwawezeshe kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kupata mitaji kwa ajili ya miradi ya nishati safi.

Ethiopia ilikuwa nchi ya kwanza kupiga marufuku uagizaji wa magari yasiyokuwa ya umeme ikiwa sehemu ya kufikia lengo lake la kuwa na hewa safi 2050.

Maelfu ya wajumbe

Umeme wote wa Ethiopia unatokana na nishati mbadala tangu 2022.

Maeneo ya kongamano ya COP hukubaliwa kwa zaidi ya mwaka mmoja kabla ya mkutano wenyewe, ili kutoa nafasi kwa mwenyeji kujiandaa kupokea maelfu ya wajumbe.

Maandalizi ya kongamano la mwaka huu Belem, Brazil, yamegubikwa na kupanda kwa bei za maeneo ya kukaa, huku mataifa maskini yakionya kuwa huenda wakashindwa kuhudhuria kutokana na gharama hizo kubwa.

Australia na Uturuki wanawania kuwa mwenyeji wa mkutano wa mwakani COP31.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us