AFRIKA
1 dk kusoma
Morocco yailiza Tanzania kufuzu kwa nusu fainali za CHAN 2024
Morocco imeifikisha kikomo safari ya Tanzania ya CHAN 2024 baada ya kuifunga 1-0 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam Ijumaa usiku.
Morocco yailiza Tanzania kufuzu kwa nusu fainali za CHAN 2024
tokea masaa 9

Goli la Oussama Lamlaoui la dakika ya 65 liliwanyamazisha mashabiki wa Tanzania waliokuwa wamejaa katika uwanja huo wa nyumbani.

Tanzania, waliingia kwenye hatua hii wakiwa na matumaini juu kutokana na kupita hatua ya makundi wakiwa hawajafungwa hata mechi moja, na licha ya juhudi za Clement Mzize na Feisal Salum (Fei Toto), golikipa wa Morocco El Mehdi Al Harrar alifanikiwa kulinda lako vyema.

Jitihada za Tanzania

Taifa Stars waliendeleza mashambulizi, lakini Morocco ikawa tayari imejizatiti na kuhakikisha kuwa hakuna atakayepenya kwenye lango lake.

Ndoto ya Tanzania ya kuwa timu inayoshiriki CHAN kwa mara ya kwanza kufuzu kwa nusu fainali tangu Madagascar kufanya hivyo 2022 ikatibuka.

Sasa wenyeji wenza wawili Kenya na Tanzania wote wamefungishwa virago. Imebaki zamu ya Uganda kujuwa hatma yao Jumamosi watakapocheza dhidi ya mabingwa watetezi Senegal.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us