Harambee Stars, ilipata goli katika dakika ya 48 wakiwa na imani ya kufuzu kwa nusu fainali katika michuano ya bara kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha miaka 38.
Lakini Madagascar ikasawazisha katika dakika ya 69 kupitia penati na kufanya matokeo kuwa 1-1. Mechi hiyo ilichezwa kwa dakika 120, ambapo matokeo yalikuwa hiyo hiyo sare.
Baadaye wakalazimika kupiga penati kutafuta mshindi atakayefuzu nusu fainali. Madagascar ilipata ushindi wa penati 4-3 za Kenya.
Uwanja wa Kasarani, jijini Nairobi ulijaa mashabiki wa Kenya ambao walikuwa na matumaini kwamba timu yao itaendeleza matokeo mazuri kama ilivyokuwa katika hatua za makundi.
Madagascar wanaingia nusu fainali wakijulikana kama ‘‘wauaji wa magwiji’’ barani Afrika, kutokana na huwa wanapewa nafasi ndogo lakini wakifika uwanjani wanapata matokeo ya kuridhisha dhidi ya mibabe ya soka.