Shirika la Mwezi Mwekundu la Somalia linawapa mafunzo ya huduma ya kwanza vijana kwa msaada wa shirika la Mwezi Mwekundu la Uturuki.
Shirika la Mwezi Mwekundu la Somalia linaendeleza miradi kwa lengo la kukabiliana na mahitaji ya msingi katika jamii kwa kushirikiana na mashirika ya nchini humo na ya kimataifa.
Mafunzo ya huduma ya kwanza na afya ni muhimu kwa jamii ambazo zimeathiriwa na migogoro na majanga, waandaaji wanasema.
Shirika la Mwezi Mwekundu la Uturuki linatoa msaada kwa vijana na taasisi nchini Somalia ikiwa moja ya washirika muhimu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mwezi Mwekundu la Somalia Mohammed Abdi Warsame na mkufunzi Ferhiye Abdullahi Hasan walieleza umuhimu wa mafunzo ya huduma ya kwanza kwa ushirikiano na Shirika la Mwezi Mwekundu la Uturuki katika mahojiano tofauti na shirika la Anadolu.
Waliopewa mafunzo wameridhika
"Tunawafunza watu. Tumechagua eneo karibu na ofisi yetu ya uratibu kwa sababu lilikuwa eneo ambalo limeathirika zaidi na milipuko, migogoro, na mashambulizi nchini ," Warsame alisema.
Alisisitiza kuwa umuhimu wa kuwapa vijana mafunzo na uzoefu, akisema, "Tunawafunza vijana kujiunga na jamii na kujitegemea."
Kuungwa mkono na Shirika la Mwezi Mwekundu la Uturuki ni muhimu sana, na Warsame akatoa shukrani zake, akisema, "Tunashkuru taifa la Uturuki na watu wake."
Aliongeza: "Ujumbe wa Shirika la Mwezi Mwekundu wa Uturuki umekuwa mshirika wetu rasmi kama Shirika la Mwezi Mwekundu la Somalia. Tungependa kuwashkuru, taifa la Uturuki na watu wake kwa msaada wao."
Mkufunzi Ferhiye Abdullahi Hasan alisema jumla ya watu 945 wamepata mafunzo ya huduma ya kwanza kufikia sasa.
Alieleza kuwa wote waliopata mafunzo, wanatoka maeneo mbali mbali na katika umri tofauti, na wamezungumzaia kuhusu kuridhishwa kwao na mafunzo hayo.