AFRIKA
1 dk kusoma
Maambukizi zaidi 100,000 ya kipindupindu Sudan ndani ya mwaka 1 huku kukiwa na njaa: UN
'Sudan inakabiliwa na janga baya la njaa duniani, huku kipindupindu kikiongezeka,’shirika la OCHA limesema
Maambukizi zaidi 100,000 ya kipindupindu Sudan ndani ya mwaka 1 huku kukiwa na njaa: UN
tokea masaa 14

Zaidi ya maambukizi 100,000 ya kipindupindu yameripotiwa katika taifa la Sudan kwenye kipindi cha mwaka mmoja uliopita, Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya misaada kwa watu (OCHA) ilisema Jumatatu. 

“Sudan inakabiliwa na janga baya la njaa kote duniani, huku kipindupindu kikiongezeka. Njaa kali imethibitishwa katika baadhi ya sehemu za nchi,” OCHA imesema katika taarifa kwenye mtandao wake wa X wa Marekani. 

“Hatuwezi kusimama tu hapa, watu wa Sudan wanahitaji msaada,” iliongeza, akiutaja mlipuko wa kipindupindu “kuwa mkubwa” katika miaka ya hivi karibuni. 

Kulingana na Wizara ya Afya ya Sudan, watu wasiopungua 2,561 wamefariki tangua kuanza kwa mlipuko wa kipindupindu Agosti 2024. 

Matatizo ya mlipuko wa kipindupindu yanakuja huku jeshi likikabiliana na wapiganaji wa RSF vilivyosababisha mauaji ya watu zaidi ya 20,000 na kuwaondoa wengie milioni 14 katika makazi yao tangu Aprili 2023, kulingana na Umoja wa Mataifa na serikali za mitaa. Hata hivyo utafiti kutoka vyuo vikuu vya Marekani, vinakadiria kuwa idadi ya waliouawa huenda ikawa 130,000.


CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us