UTURUKI
2 dk kusoma
Emine Erdogan atoa wito wa ushirikiano thabiti wa kitamaduni, mazingira katika hafla ya SCO
Wake wa marais wa Uturuki, Nepal, Armenia, Malaysia, Mongolia, Azerbaijan, Iran, Misri, na Uzbekistan, pamoja na binti wa rais wa Iran, walihudhuria hafla ya kitamaduni pembeni mwa kongamano la SCO.
Emine Erdogan atoa wito wa ushirikiano thabiti wa kitamaduni, mazingira katika hafla ya SCO
"Nina matumaini kuwa mikutano hii yenye umuhimu itaimarisha zaidi ushirikiano wa mataifa yetu,” Emine Erdogan alisema. / Ofisi ya Rais wa Uturuki
tokea masaa 7

Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan ameshiriki katika hafla ya kitamaduni iliyoandaliwa na Mke wa Rais wa China Peng Liyuan pembeni mwa Kongamano la 25 la Baraza ka Wakuu wa Nchi la SCO.

Alikaribishwa vyema na Peng alipowasili kwenye hafla hiyo, ambayo iliwaleta pamoja wake za marais waliopiga picha ya pamoja kabla ya kuendelea na ratiba ya hafla ya kitamaduni iliyoonyesha tamaduni mbalimbali za mataifa yanayoshiriki kwenye kongamano hilo, Ofisi ya Rais wa Uturuki ilisema katika taarifa siku ya Jumatatu.

Wake wa marais wa Nepal, Armenia, Malaysia, Mongolia, Azerbaijan, Iran, Misri, na Uzbekistan, pamoja na binti wa rais wa Iran, pia walikuwepo.

Hafla hiyo ilikuwa fursa ya washiriki kubadilishana maoni kuhusu urithi wa kitamaduni na masuala yanayotuleta pamoja, taarifa ilisema.

Kufuatia hafla hiyo, Emine Erdogan alieleza mtazamo wake katika mtandao wa kijamii, akieleza furaha yake kwa kushiriki mkutano ulioandaliwa na Peng.

“Katika ratiba hii maalum ambapo tumeona utamaduni wa Tianjin na utajiri wake wa majengo ya kale, tumekuwa na mazungumzo ya kirafiki na tukabadilishana maoni kwa masuala yanayotuleta pamoja kama amani, familia, mazingira na ushirikiano wa kitamaduni ,” alisema.

“Nina matumaini kuwa mikutano hii yenye umuhimu itaimarisha zaidi ushirikiano wa mataifa yetu.”

Rais wa China Xi Jinping alikuwa mwenyeji wa mkutano huo wa siku mbili wa viongozi wa SCO pamoja na “SCO plus,” uliowaleta pamoja viongozi 20 wa nchi na serikali, pamoja na viongozi wa mashirika ya kimataifa.

Ilikuwa kongamano kubwa zaidi la SCO pamoja na China kuwa wenyeji wa mara ya tano wa kongamano hilo tangu SCO ilipoundwa 2001.

CHANZO:TRT World
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us