AFRIKA
2 dk kusoma
AU yaeleza wasiwasi wake kuhusu makubaliano ya wahamiaji ya Marekani na mataifa ya Afrika
Makubaliano ya kuwapeleka wahamiaji maeneo mengine ni sehemu ya kukwepa majukumu ya uhamiaji na kuwaweka watu katika hatari ya mateso na ukiukwaji wa haki zao za msingi,’ shirika la haki la AU limesema
AU yaeleza wasiwasi wake kuhusu makubaliano ya wahamiaji ya Marekani na mataifa ya Afrika
tokea masaa 10

Shirika la haki la Umoja wa Afrika lilieleza wasiwasi wake siku ya Jumatatu kuhusu makubaliano ya Rwanda na Uganda na Marekani ambayo yatawezesha kupelekwa kwa wahamiaji katika nchi hizo.

Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (ACHPR), katika taarifa, iliomba Rwanda, Uganda, na mataifa mengine ya Afrika kuhakikisha uwazi katika makubaliano yao ya kuwachukua wahamiaji, kulinda haki za wahamiaji, na kuepuka sera ambazo zitafanya bara hilo kuwa “jalala” kwa watu wanaofukuzwa bila utaratibu.

ACHPR iliyaita makubaliano hayo “kuwa sehemu ya kukwepa majukumu yao ya uhamiaji na kuwaweka watu katika hatari ya mateso na ukiukwaji wa haki zao za msingi.”

Shirika hilo la AU linasema kuwa uhamiaji huo unaweza kukiuka misingi ya haki za wahamiaji, marufuku ya kuwaondoa watu kwa pamoja, na haki za heshima na wanaotaka hifadhi ya kisiasa chini ya mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu na makubaliano mengine ya kimataifa na kikanda.

Mwezi huu Uganda ilikuwa nchi ya hivi karibuni kufikia makubaliano ya “muda” na Marekani kukubali watu wa mataifa ya tatu ambao wamenyimwa hifadhi nchini Marekani.

Nchi hiyo ya Afrika Mashariki inaungana na Rwanda, Eswatini, na Sudan Kusini, ambazo zimekubali kuchukuwa wahamiaji kutoka Marekani tangu serikali ya Rais Donald Trump ilipoamua kuwa Afrika ndiyo itakuwa sehemu ya kuwapeleka wahamiaji hao.

Wiki iliopita, Rwanda ilithibitisha kufika kwa kundi la kwanza la wahamiaji saba kutoka Marekani, wiki kadhaa baada ya mamlaka kusema kuwa serikali ilikubali kuwapokea wahamiaji 250.

Mwezi Julai, Trump alitumia mkutano wake katika Ikulu ya White House na marais wa Gabon, Guinea-Bissau, Liberia, Mauritania, na Senegal kuwaomba viongozi wa mataifa hayo kuchukuwa wahamiaji waliotimuliwa Marekani.

Majibu kutoka nchi za Afrika yamekuwa tofauti, huku wengine wakikubali, na nchi kama Nigeria, ikikataa shinikizo la kuwapokea raia wa Venezuela waliofukuzwa Marekani.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us