AFRIKA
2 dk kusoma
Afisa polisi wa Kenya afariki katika ajali ya barabarani Haiti
Maafisa polisi wanane wa Misheni ya Usaidizi ya Usalama wa Kimataifa (MSS) nchini Haiti wamejeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani Jumapili, huku afisa mmoja wa Kenya akifariki dunia.
Afisa polisi wa Kenya afariki katika ajali ya barabarani Haiti
Kati ya maafisa polisi 2,500 waliotarajiwa kupelekwa na MSS nchini Haiti, takriban 1,000 kutoka mataifa sita pekee ndio wamepelekwa / Reuters
tokea masaa 5

Kwa mujibu wa msemaji wa MSS, Jack Ombaka, tukio hilo lilitokea majira ya saa 11 jioni likihusisha magari mawili ya aina ya MaxxPro, ambapo gari moja lilipokuwa likivuta jingine lilipata hitilafu ya kiufundi.

Maafisa waliojeruhiswa pamoja na raia walipelekwa katika Hospitali ya Lambert Santé iliyopo Pétion-Ville, ambapo afisa wa Kenya na raia mmoja walifariki dunia.

“Maafisa wa polisi wanane wa MSS walijeruhiwa, wanne wakiwa katika hali mbaya hivyo wanahitaji kuhamishwa kwa ajili ya kupata matibabu maalum nchini Jamhuri ya Dominika baada ya kupokea huduma ya kwaza katika Hospitali ya Aspen Level 2,” alisema Ombaka katika taarifa yake.

Aidha, Ombaka alitoa rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha baada ya tukio hilo.

Huduma ya Polisi Kitaifa (NPS) imethibitisha kuwa MSS kwa kushirikiana na Polisi wa Kitaifa wa Haiti (HNP) wanapanga kurejesha maiti ya afisa huyo nchini Kenya na kuhakikisha majeruhi wanaendelea kupata huduma bora za matibabu.

Familia wa afisa huyo pia wamepatiwa taarifa kuhusu tukio hilo.

Misheni ya MSS, inayoongozwa na Kenya, iilipelekwa Haiti zaidi ya mwaka mmoja uliopita, lakini hali nchini humo inaendelea kuwa mbaya, hasa katika mji mkuu Port-au-Prince ambao karibu kwa sehemu kubwa uko chini ya udhibiti wa makundi ya uhalifu.

Kati ya maafisa polisi 2,500 waliotarajiwa kupelekwa na MSS nchini Haiti, takriban 1,000 kutoka mataifa sita pekee ndio wamepelekwa, ikiwa ni pamoja na zaidi ya 700 kutoka Kenya.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us