UTURUKI
2 dk kusoma
Erdogan anataka ushirikiano thabiti wa SCO, apongeza msimamo kuchukuwa hatua kwa pamoja
Akizungumza katika kongamano la SCO nchini China, Rais wa Uturuki Erdogan ameridhishwa na hatua zilizopigwa hivi karibuni zenye lengo la kupata amani ya kudumu na usalama katika maeneo ya Caucasus ya Kusini na Asia ya Kati.
Erdogan anataka ushirikiano thabiti wa SCO, apongeza msimamo kuchukuwa hatua kwa pamoja
Erdogan ameridhishwa na hatua za hivi karibuni katika kuleta amani ya kudumu na usalama maeneo ya Caucasus ya Kusini na Asia ya Kati. / Reuters
tokea masaa 5

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema ana matumaini ya kuimarisha ushirikiano na Shanghai Cooperation Organisation (SCO), akiutaja ushirikiano huo kama jukwaa “linalowakilisha utamaduni wa kupata suluhu ya pamoja kwa matatizo.”

Akizungumza katika kongamano la 25 la Baraza la Wakuu wa Nchi huko Tianjin, China siku ya Jumatatu, Erdogan aliuelezea ushirikiano huo kama “muhimu” kwa kuimarisha usalama wa nishati na kuendeleza ushirikiano wa kimkakati katika masuala ya miundombinu.

Pia alieleza kuridhishwa kwake na hatua zilizopigwa hivi karibuni zenye lengo la kupata amani ya kudumu na usalama katika maeneo ya Caucasus ya Kusini na Asia ya Kati.

Kongamano hilo la siku mbili la SCO, ambalo lilianza siku ya Jumapili, linaadhimisha mwaka wa tano kwa China kuwa wenyeji tangu kuanzishwa kwa jukwaa hilo 2001.

Mapema, Erdogan alikutana na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin pembeni mwa kongamano hilo.

'Jukumu letu la pamoja'

Akizungumzia kuhusu migogoro duniani, Erdogan alishtumu vita vinavyoendelea Gaza. “Hakuna sababu ya kushindwa kusitisha ukatili wa miezi 23 Gaza, ambapo watoto wachanga, watoto, na wazee wanakufa kwa njaa,” alisema.

Alitoa wito kwa jamii ya kimataifa kutumia Umoja wa Mataifa kama jukwaa la kutafuta haki duniani, akieleza kama “jukumu letu la pamoja” la kukabiliana na miaka mingi ya dhulma dhidi ya watu wa Palestina.

Israel imewaua Wapalestina zaidi ya 63,500 Gaza tangu Oktoba 2023. Vita vya Israel vimeharibu eneo hilo, ambalo linakabiliwa na njaa kali.

Kuhusu Syria, Erdogan alisisitizaa kuendelea kuwaunga mkono katika ujenzi wa nchin yao huku wakihakikisha kuheshimu mipaka yao na umoja wao wa kisiasa, akisema juhudi kama hizo zinasaidia kanda nzima.

Pia alisisitiza kuwa Uturuki itapinga juhudi zozote ambazo zinatishia usalama wa Syria au uhuru wake.

Erdogan alihitimisha kwa kueleza dira pana ya sera ya mambo ya nje ya Uturuki, akisisitiza umuhimu wa majadiliano, diplomasia, na ushirikiano kwa misingi ya kuheshimu mipaka ya nchi zote.

Alieleza umuhimu kuimarisha nishati na kuunganisha watu kwa usalama wa dunia, maendeleo ya kiuchumi, na ukuaji endelevu.

CHANZO:TRT World
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us