AFRIKA
2 dk kusoma
Mwanasiasa wa upinzani Uganda akataa kufika mahakamani akidai jaji ana upendeleo
Kesi ya Kizza Besigye na msaidizi wake, Obed Lutale, ilitakiwa kuanza kusikilizwa Jumatatu baada ya kuchelewa kwa miezi kadhaa, lakini washtakiwa wote waliamua kususia kesi hiyo baada ya hakimu, Emmanuel Baguma kukataa kujiondoa kwenye shauri hilo.
Mwanasiasa wa upinzani Uganda akataa kufika mahakamani akidai jaji ana upendeleo
Kiiza Besigye na msaidizi wake amekuwa kizuizini tangu Novemba 2024/ Picha Reuters / AP
tokea masaa 12

Mwanasiasa mkongwe nchini Uganda aliye kizuizini, Kizza Besigye alisusia kuanza kwa kesi yake ya uhaini siku ya Jumatatu, akimtuhumu jaji kiongozi kwa upendeleo, wakili wake alisema.

Kuzuiliwa kwa Besigye kwa miezi kadhaa kumeangazia rekodi ya haki za binadamu ya Rais Yoweri Museveni kabla ya uchaguzi wa mapema mwaka ujao ambapo Museveni, 80, anaomba kuchaguliwa tena.

Kesi ya Besigye na msaidizi wake, Obed Lutale, ilitakiwa kuanza kusikilizwa Jumatatu baada ya kuchelewa kwa miezi kadhaa, lakini washtakiwa wote waliamua kususia kusikilizwa kwa kesi hiyo baada ya hakimu, Emmanuel Baguma kukataa kujiondoa, wakili wao Eron Kiiza aliambia shirika la habari la Reuters.

Mawakili wa Besigye walitaja uamuzi wa Baguma wa kumnyima dhamana Besigye kama msingi wa tuhuma za upendeleo.

Msemaji wa mahakama James Ereemye Mawanda alisema hakuna uhalali wa shutuma hizo za upendeleo na kuthibitisha kuwa Baguma alikataa kujiuzulu.

Hakimu Baguma hakupatikana kutoa maoni mara moja.

“Besigye na Lutale walichukua uamuzi wa kutofika mbele ya Jaji Baguma,” wakili Kiiza alisema.

"Hana uwezo wa kutoa haki kwa haki na bila upendeleo kama inavyotakiwa na katiba na mantiki," Kiiza aliongeza.

Aliyekuwa mshirika na daktari wa binafsi wa Museveni, Besigye amesimama dhidi ya Museveni na kushindwa katika uchaguzi mara nne.

Kwa Sasa hajaonyesha nia ya kutaka kugombea tena.

Aliwekwa kizuizini pamoja na msaidizi wake Novemba mwaka jana katika nchi jirani ya Kenya na kurejea Uganda ambapo wote wawili walishtakiwa kwa uhaini na makosa mengine, awali katika mahakama ya kijeshi kabla ya kesi hiyo kuhamishiwa katika mahakama ya kiraia.

Anakanusha mashtaka yote.


CHANZO:TRT Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us