Neno 'ukoloni' na 'ukoloni mamboleo' ni mambo mawili muhimu ambayo yametoa mtazamo ya siasa za dunia za karne ya 19.
Ukoloni unaweza ukasemekana kuwa "mataifa’ yaliyochukuliwa na nchi za nje yaliyopo nje ya mipaka yake, hasa kwa kutumia nguvu ya kijeshi, na kuanzisha utawala huko, kujinufaisha kisiasa, kiuchumi na kitamaduni.".
Ukoloni mamboleo ni siasa zaidi. Mitazamo yote yana historia ubepari, na ina uhusiano wa kihistoria na itikadi.
Bila shaka, mfumo wa mapinduzi ya viwanda wa Uingereza, ambao uliupa ubepari mtazamo wake wa sasa.
Miongoni mwa nchi zilokuwa na uwezo kuanza kuenea kutoka bara Ulaya ahdi duniani kote, Uingereza ilikuwa ya kwanza ikiwa na shughuli zake za kibiashara, na jeshi lake la wanamaji, ambayo yalikuwa matokeo ya ukubwa wa ukoloni wake.
Ukoloni wa Biashara Huru
Wakati wa kipindi hiki “Ukoloni wa Biashara Huru” (1830-1880), inasemekana kuwa Uingereza ilijenga nguzo ya uhusiano wa kibepari ambayo baadaye ilikuja kuwapa uwezo wa kuwa na maeneo mengi.
Mbali na India, ukoloni wa Uingereza Misri na Sudan, unafanana.
Ukweli ni kuwa, Uingereza, ambao walifnaikiwa kuchukuwa udhibiti wa Sudan na kuharibu Taifa la Mahdi mwishoni mwa 1898, na kupata eneo jipya la himaya ya ukoloni wao kwa usalama wa Misri na kufaidika na utajiri wa Sudan.
Mgawanyiko wa Kaskazini na Kusini
Mgawanyiko wa kaskazini na kusini ambao ukoloni wa Uingereza ulianzisha nchini Sudan, ulikuwa tofauti na Misri Egypt, ilikuwa maamuzi ya kiutawala.
Waislamu Waarabu wakiwa upande wa kaskazini na makabila ya Kiafrika ambayo hayakuwa na dini upande wa kusini Sudan ilikuwa nchi ambayo makabila zaidi ya mia mbili yalikuwa yanaishi pamoja, huku lugha ziadi ya mia moja zikizungumzwa.
Hata hivyo, tofauti na Misri, mfumo mgumu wa Sudan, ukiwa na makabila mbali mbali na makundi kadhaa ya kidini, ulichelewesha utawala wa Uingereza katika maeneo haya kwa miaka mengi.
Mmoja wa mifano ya haya ni kwamba 1924, miaka ishirini na tano baada ya kuanzishwa kwa utawala wa pamoja wa Uingereza kwa Misri wenye makao yake Khartoum 1899, mipaka ya Darfur, moja ya maeneo muhimu Sudan, ilibainishwa wazi.
Moja ya suala ambalo Uingereza ilikabiliana nalo Sudan ilikuwa lile la usalama.
Sera ya uwili ambayo iligawanya Sudan kusini na kaskazini, inaweza kusema kuhusu madhila wanayopitia Sudan leo.
Siasa za kidini
Nchini Sudan chini ya utawala wa Uingereza, utaratibu kama wa kuteuwa wanajeshi na watumishi wa umma ulitekelezwa kwa misingi ya siasa za kidini wakigawanya kaskazini na kusini.
Uingereza ilijaribu kujitenga na maneno kama dhidhi ya Uislamu katika upande wenye Waarabu wengi walio Waislamu wa kaskazini mwa Sudan, ambapo kulikuwa na mifumo miwili tofauti ya kikabila na kidini.
Pamoja na hayo wamishenari wa Kikristo kutoka Marekani, hawakuruhusiwa kuingia kaskazini. Kusini, Uingereza ilifungua eneo hilo kusini, ambalo lilikuwa na makabila ya Kiafrika yenye imani za kitamaduni.
Ili kuzuia kuenea kwa utamaduni wa Kiislamu kusini mwa Sudan, matumizi ya maandishi ya Kiarabu na hata kuvaa mavazi ya Kiarabu kulipigwa marufuku.
Katika kipindi cha baada ya 1914 nchini Sudan, suala lilokuwa na utata zaidi kwa Uingereza lilikuwa mapambano yaliyoungwa mkono na dola ya Ottoman yakiongozwa na Ali Dinar. Ali Dinar, alikuwa sultan wa Darfur na mtawala wa himaya ya Keira.
Pamoja na hayo, Utawala wa Ottoman uliwaunga mkono zaidi watu wa Darfur dhidi ya Uingereza, kwa kuwapa silaha, na fedha.
Wakati Uingereza ikipambana na viongozi wa Taifa na makundi ndani ya Sudan, pia katika miaka ya 1930 waliangalia masuala kama vile ya mpaka wa Sudan na Abyssinia na uvamizi wa Italia Abyssinia.
Katika uchaguzi wa 1953, uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia uliofanyika kwa kushiriki vyama vya kwanza vya kisiasa ambavyo vilianza kujipanga katika miaka ya 1940, chama cha National Unity Party kilishinda uchaguzi na mara moja kikaanza kufanya kazi ya mabadiliko ya Sudan kwa makubaliano ya 1953 yaliyotiwa saini kati ya Uingereza na Misri.
Kwa makubaliano hayo yaliyofikiwa na Uingereza, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Sudan ilifikia kikomo mwishoni mwa 1955, huku bendera ya Sudan ikibadilishwa na utawala wa pamoja wa Uingereza na Misri, ambayo ilikuwa inapepea mjini Khartoum tangu 1899, Januari 1, 1956.
Mwandishi, Ali Bilgenoğlu ni profesa katika Chuo Kikuu cha Aydın Adnan Menderes University, idara ya Uhusiano wa Kimataifa.
Kanusho: Maoni ya mwandishi hayaakishi maoni, mitazamo na sera za uhariri za TRT Afrika.