ULIMWENGU
1 dk kusoma
Tetemeko kubwa la ardhi lazikumba Chile na Argentina
Hakuna vifo, wala madhara yoyote yaliyoripotiwa hadi kufikia sasa.
Tetemeko kubwa la ardhi lazikumba Chile na Argentina
Chile na Argentina zakumbwa na tetemeko la ardhi./Picha:Wengine
22 Agosti 2025

 Mamlaka nchini Chile zimetoa tahadhari ya uwezekano wa kutokea kwa tsunami kufuatia tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo.

Chile, pamoja na Argentina zilikumbwa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha 7.5, siku ya Alhamisi, kulingana na Taasisi ya Jiolojia ya Marekani.

Tetemeko hilo lilitokea majira ya saa 5:16 usiku(kwa saa za Afrika Mashariki), likiwa na kina cha kilomita 10.8.

Aidha, tetemeko hilo linaripotiwa kutokea katika eneo la kusinimashariki mwa Ushuaia nchini Argentina.

CHANZO:AP
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us