AFRIKA
1 dk kusoma
Jeshi la Sudan lakanusha kushambulia kwa bomu msafara wa msaada wa WFP Darfur
Jeshi la Sudan limekanusha madai ya wapiganaji wa RSF kuwa limefanya mashambulizi ya angani dhidi ya msafara wa misaada wa shirika la Mpango wa Chakula (WFP) uliokuwa unapeleka misaada Darfur.
Jeshi la Sudan lakanusha kushambulia kwa bomu msafara wa msaada wa WFP Darfur
Jeshi la Sudan, chini ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, limekanusha madai ya RSF kuwa jeshi limeshambulia msafara wa misaada Darfur. / Wengine
tokea masaa 4

Jeshi la Sudan limekanusha madai ya wapiganaji wa RSF kuwa limefanya mashambulizi ya angani kwa msafara wa misaada wa shirika la WFP lililokuwa likipeleka misaada Darfur.

Katika taarifa iliyosambazwa kwenye mtandao wa kijamii wa X, jeshi limesema kuwa madai ya RSF yalikuwa ya “uongo” na yenye lengo la kuficha kile walichokieleza kuwa ni mashambulizi ya wapiganaji dhidi ya msafara katika mji wa Mellit.

Taarifa hiyo imeshtumu RSF kwa kuendeleza “ukiukaji” tangu kuanza kwa mapigano. Pia ilidai kuwa wapiganaji wamefanya kambi za wakimbizi wa ndani kama maeneo ya mafunzo wakisaidiwa na mamluki.

“Serikali, ambayo ilifunguwa njia ya misaada, ikiwemo mpaka wa Adré wa Sudan na Chad, haiwezi katika mazingira yoyote kulenga msafara unaobeba misaada kuwapelekea watu wetu,” jeshi limesema.

Jeshi limeapa kuendelea kupigana dhidi ya RSF

Jeshi limeapa kuendeleza operesheni dhidi ya RSF na kile ilichosema kuwa wasaidizi wake kutoka nje “hadi pale taifa litakuwa huru kutokana na uhalifu.”

Katika wiki za hivi karibuni, RSF imepoteza maeneo kwa jeshi, ambalo limechukuwa udhibiti wa sehemu kadhaa, ikiwemo Khartoum na majimbo ya White Nile.

Wapiganaji wanadhibiti sehemu za Kaskazini na Magharibi mwa Kordofan, baadhi ya sehemu ya Kordofan Kusini na Blue Nile, na majimbo manne kati ya matano ya Darfur.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us