AFRIKA
1 dk kusoma
Idadi ya vifo yafikia 30 katia shambulio la msikiti Nigeria
Serikali imesema kuwa mashirika ya usalama yamepelekwa katika eneo hilo ili kurudisha utulivu.
Idadi ya vifo yafikia 30 katia shambulio la msikiti Nigeria
Polisi wamepelekwa kurudisha utulivu katika eneo hilo. / Reuters
20 Agosti 2025

Watu wenye silaha wameua takriban watu 30 katika shambulio la msikiti kaskazini magharibi mwa Nigeria, hayo ni kwa mujibu wa mkazi na mbunge wa eneo hilo, na kuongeza idadi ya waliokufa kutoka 13.

“Watu wenye silaha,” makundi ya uhalifu kama wanavyojulikana, wameshambulia msikiti uliopo katika mji wa Unguwar Mantau siku ya Jumanne, katika jimbo la Katsina.

“Waumini tisa waliuliwa hapo kwa hapo na wengine wengi walikufa baadae. Idadi za hivi punde za waliopoteza maisha ni 32,” amesema Nura Musa, mkazi wa eneo hilo siku ya Jumatano.

Mwanasiasa wa eneo hilo Amimu Ibrahim ameliambia Bunge la Katsina siku ya Jumanne kwamba watu 30 waliuawa.

Taarifa ya Kamishna wa Jimbo la Katsina wa Usalama na Masuala wa Ndani, Dkt Nasir Muazu, amesema kuwa shambulio hilo ni kulipiza kisasi kwa ufanisi wa ulinzi wa jamii uliofanyika siku mbili zilizopita, kwa sababu watu wa Unguwan Mantau waliwashambulia magaidi na kuwaua wengi wao.

Kwa upande wake, serikali imesema, vikosi vya ulinzi tayari vimepelekewa kwa ajili ya kurudisha hali ya utulivu.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us