AFRIKA
1 dk kusoma
Watu wasiopungua 22 wanaaminika kufariki katika ajali ya boti Nigeria
Watu wasiopungua 22 wanaaminika kufariki baada ya boti kuzama kaskazini magharibi mwa Nigeria, shirika la huduma ya dharura la nchi hiyo limesema siku ya Jumatano.
Watu wasiopungua 22 wanaaminika kufariki katika ajali ya boti Nigeria
Nigeria inasema kuwa watu wasiopungua 22 wanaaminika kufariki siku chache baada ya boti lao kuzama katika jimbo la Sokoto Agosti 17, 2025. / AP
20 Agosti 2025

Watu wasiopungua 22 wanaaminika kufariki baada ya boti kuzama kaskazini mashariki mwa Nigeria, shirika la huduma la dharura la nchi lilisema siku ya Jumatano.

Boti hiyo ilikuwa imewabeba wakulima 50 na wafanyabiashara waliokuwa wanaelekea kwenye soko ilipozama katika jimbo la kaskazini magharibi la Sokoto siku ya Jumapili.

Watu ishirini na tano waliokolewa muda mfupi baada ya ajali hiyo na wafanyakazi wa dharura, Shirika la Taifa la Dharura (NEMA) limesema, na miili mitatu ilipatikana siku ya Jumanne.

Watu ishirini na mbili hawajulikani waliko lakini juhudi za uokoaji zimekamilika, amesema mkuu wa operesheni wa NEMA huko Sokoto, Aliyu Kafindangi.

Shughuli za uokoaji zimesitishwa

"Shughuli za uokoaji zimesitishwa kwa sababu inaaminika kuwa baada ya saa 24, hakuna uwezekano wa kupatikana manusura," Kafindangi aliliambia shirika la habari la eneo hilo siku ya Jumatano.

Wakulima wasiopungua 16 walifariki katika ajali kama hiyo mwezi Agosti 2024 wakati boti lao ambalo lilikuwa linawapeleka kwenye mashamba yao ya mpunga kuzama katika jimbo la Sokoto.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us