SIASA
2 dk kusoma
Tanzania: Chama cha ACT Wazalendo kushiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025
Kulingana na kiongozi wa chama hicho Dorothy Semu, kufanya hivyo itakuwa ni sawa na kuwapa chama tawala cha CCM nafasi ya ushindi.
Tanzania: Chama cha ACT Wazalendo kushiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025
Dorothy Semu ametoa kauli hiyo Aprili 16, 2025 mjini Vuga, Zanzibar wakati wa kikao cha chama hicho. /Picha: ACTwazalendo
16 Aprili 2025

Chama cha upinzani Tanzania ACT Wazalendo, kimesema kuwa hakitogomea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Kulingana na kiongozi wa chama hicho Dorothy Semu, kufanya hivyo itakuwa ni sawa na kuwapa chama tawala cha CCM nafasi ya ushindi.

Semu ametoa kauli hiyo Aprili 16, 2025 mjini Vuga, Zanzibar wakati wa kikao cha chama hicho.

“Naomba kuwajulisha kuwa baada ya tafakuri ya kina, Kamati ya Uongozi ya Taifa imeamua kuwa Chama cha ACT Wazalendo kitashiriki kwenye Uhcgauzi Mkuu wa 2025 kwa nafasi zote za Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Urais wa Zanzibar, Ubunge, Uwakilishi na Udiwani,” Semu alisema.

Kulingana na kiongozi huyo wa ACT Wazalendo, huo ndio uamuzi sahihi unaopaswa kuchukuliwa na chama hicho kwa kuzingatia hali ya kisiasa nchini Tanzania na wajibu wa kimapambano ambao umebebwa na chama hicho.

Semu amesisitiza kuwa sababu ilizokisukuma chama cha ACT Wazalendo kufikia maamuzi hayo ni kiu ya kutetea na kulinda thamani ya kura na kuwa, kususia uchaguzi kutaimarisha hujuma dhidi ya demokrasia.

TRT Global - Chama kikuu cha upinzani Tanzania CHADEMA chafungiwa nje ya uchaguzi mkuu ujao

Tume Huru ya Uchaguzi ilikiondoa chama cha Chadema kutoshiriki uchaguzi mkuu na chaguzi zote ndogo kwa miaka mitano ijayo.

🔗

“CCM imeshindwa kuwakomboa Watanzania kiuchumi, kisiasa na kijamii. Bila shaka hii ni kwa sababu CCM imechoka na haiwezi tena kuwa na fikra za kuwakomboa Watanzania,” aliongeza.

Uamuzi huo unakuja baada ya chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA kususia kusaini kanuni za maadili ya uchaguzi na hivyo kuilazimu Tume Huru ya Uchaguzi nchini humo (INEC), kukizuia kushiriki Uchaguzi Mkuu ujao na chaguzi nyingine ndogo ndogo.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us