Taswira za wasafiri waliosimama kwenye mistari mirefu nyuma ya meza za uhamiaji jijini Mogadishu kwa sasa zimekuwa simulizi.
Mwanzoni mwa mwezi Septemba, serikali ya Somalia ilihamisha huduma zake za uhamiaji na kuzifanya ziwe za kidijiti.
Mfumo huo wenye kufanya kazi kwa kutumia dirisha la serikali, litamaliza adha ya matumizi ya karatasi katika huduma za usafiri.
Kati ya mwaka 2014 na 2021, Somalia ilizindua mfumo wa kuandikisha na kusajili wageni, wenye kuendana na sera za uhamiaji nchini humo pamoja na kanuni za kimataifa.
Mchakato huo usasishwa ndani ya miaka minne, na kuanzisha ari ya kwenda kidijiti.
Mifumo ya kisheria
Utaratibu huu mpya unaleta mapinduzi kwenye mfumo wa udhibiti na usimamizi wa vitengo vya uhamiaji nchini Somalia.
Kupitia viza hizi, wasafiri watahitajika kufanya usajili kwa njia ya mtandao kabla ya kuanza safari zao.
Mashirika ya ndege yatalazimika kulipa faini iwapo abiria wake watashindwa kujisajili kupitia mfumo huu.
Mchakato huu hufanya kazi kupitia hatua tatu, zikiwemo uhakiki, uthibitisho na utoaji wa vibali hivyo vya kusafiri.
Vibali hivyo hupatikana kati ya siku moja hadi tatu, na kuondoa mfumo wa zamani wa matumizi ya karatasi, ambao kwa kiasi kikubwa ulikuwa na mianya ya rushwa.
‘‘Tunatumia mfumo huu katika kuhakikisha kuwa hakuna yeyote atakayetoka wala kuingia nchini bila kufanyiwa uhakika wa taarifa zao,’’ anasema Mustafa Duhulow, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Uhamiaji na na Uraia nchini humo.
‘‘Hadi kufikia sasa, tumetoa mafunzo kwa watu 108 kwa kutumia mfumo huu,’’ anasema Dhuhulow.
Kulingana na wataalamu, mfumo utasaidia kupambana na ugaidi, usafirishaji binadamu na uhalifu wa kuvuka mipaka.
‘‘Tutahakikisha kuwa hakuna wasafiri haramu wa kuingia wala kutoka Somalia. Tunafanya kazi kwa ukaribu na washirika wetu wa kimataifa,’’ alisema Duhulow.
‘‘Kama sehemu ya vyombo vya usalama, tutahakikisha kuwa hakuna vitisho vya Al-Qaeda, ISIS, wala Al-Shabab,’’ aliongeza.
Uwazi wa kifedha
Mfumo huu mpya utahakikisha malipo yote yanafanyika kwa uwazi bila kuwepo na mianya ya rushwa.
"Huu ni wakati mzuri sana kwa nchi yetu," anasema Waziri wa Usalama wa Ndani wa Somalia, Abdullahi Sheikh Ismail Fartaag.
"Mfumo huu unawataka wasafiri kuweka wazi sababu za safari zao saa 24 kabla ya kusafiri."
Utambulisho wa kimiundombinu