AFRIKA
2 dk kusoma
Mahakama Kenya yapigia msumari sheria ya kustaafu miaka 60
Uamuzi huo ulitolewa katika kesi iliyowasilishwa na raia mmoja, ambaye alidai kuwa kuwataka wafanyakazi kustaafu wakiwa na miaka 60 - au 65 ni ukiukaji wa haki za kikatiba za usawa kwa watu wenye ulemavu.
Mahakama Kenya yapigia msumari sheria ya kustaafu miaka 60
Mahakama Kenya imakataa kubadilisha umri wa kusataafu kwa wafanyikazi/ Picha: Getty / TRT Afrika Swahili
15 Agosti 2025

Mahakama Kuu nchini Kenya imeidhinisha umri wa lazima wa kustaafu kwa wafanyakazi katika sekta ya umma na kibinafsi, ikitupilia mbali ombi lililotaka kutangaza sera hiyo kuwa kinyume na katiba.

Wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi kupitia sheria ya kustaafu ni kati ya umri wa miaka 60, au 65 kwa watu wenye ulemavu, Mahakama Kuu imesisitiza.

Jaji Lawrence Mugambi alitoa uamuzi huo katika kesi iliyowasilishwa na Charles Chege Gitau, ambaye alidai kuwa kuwataka wafanyakazi kustaafu wakiwa na miaka 60 - au 65 kwa watu wenye ulemavu - ni kulikiuka haki za kikatiba za usawa, utu na mazoea ya haki ya kazi.

"Madai kwamba umri wa lazima wa kustaafu ... unabagua kwa sababu unawafanya watu katika jamii hiyo kukosa kazi sio sahihi kabisa, ikizingatiwa kuwa sheria na kanuni zinaruhusu mwajiriwa kubakishwa kwa mujibu wa kandarasi," Jaji Mugambi alisema.

Gitau alidai sera hiyo iliimarisha dhana potofu kuhusu tija ya wafanyakazi wazee, imeshindwa kushughulikia ukosefu wa ajira kwa vijana ipasavyo, na haikuafikiana na misamaha ya kustaafu kwa majaji, wabunge, na watafiti wa vyuo vikuu.

Pia alitoa changamoto kwa Tume ya Utumishi wa Umma (PSC) kupanua sera hiyo kwa sekta binafsi bila kuungwa mkono wazi na kisheria.

"Jukumu la kuweka masharti ya huduma, ikiwa ni pamoja na umri wa kustaafu, linabaki kwa mwajiri," Jaji Mugambi alisema, akibainisha kuwa sera hiyo inasawazisha fursa kwa wafanyakazi wazee na vijana wanaotafuta ajira.

Jaji alisema pia kuwa kuna umri tofauti wa kustaafu kwa majukumu fulani - kama vile majaji, wabunge, na watafiti wakuu - unategemea mahitaji ya kipekee ya kazi na haijumuishi ubaguzi.

CHANZO:TRT Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us