AFRIKA
2 dk kusoma
Kuridhia kwa serikali ya Eswatini kupokea waliotimuliwa Marekani kwapinga mahakamani
Wanaharakati wa Eswatini wameiomba mahakama kuu kuamua kuwa kinyume cha katiba hatua ya nchi hiyo kukubali kuwapokea raia watano wa kigeni ambao walifukuzwa Marekani.
Kuridhia kwa serikali ya Eswatini kupokea waliotimuliwa Marekani kwapinga mahakamani
Serikali ya Eswatini inasema wafungwa wa Marekani walioko kwao siyo hatari kwa umma. / Picha: Reuters
tokea masaa 9

Wanaharakati wa Eswatini wameitaka mahakama kuu kuamia kuwa ni kinyume cha katiba kwa nchi yao kukubali kuwapokea raia watano wa nje ambao walitimuliwa kutoka Marekani baada ya kuwepo gerezani kwa hatia ikiwemo mauaji.

Wanaume hao kutoka Vietnam, Laos, Yemen, Cuba na Jamaica walisafirishwa hadi katika taifa hilo la Kusini mwa Afrika kwa ndege ya kijeshi ya Marekani mwezi Julai ikiwa ni sehemu ya mpango wa Marekani wa kuwapeleka wahamiaji katika mataifa ya tatu.

Katika shauri la dharura kwenye mahakama kuu ya Eswatini, mashirika matatu ya kisheria na ya kiraia yanasema makubaliano ni kinyume cha katiba kwa sababu hayakuwa yamewekwa wazi na hakukuwepo na mashauriano ya umma au bunge.

Walitaka serikali ya Eswatini kuweka wazi makubaliano kamili na Marekani.

Madai ya 'uongozi kupita mipaka'

"Mazingira ambayo makubaliano hayo yamefanyika yanatia wasiwasi kuhusu uongozi wa nchi kupita mipaka, haki za binadamu na usalama wa nchi," walisema katika taarifa wakati wakitangaza hatua ya kuelekea mahakamani.

Watano hao waliopelekwa nchini humo wamefungiwa katika maeneo ya peke yako katika gereza lenye ulinzi mkali ambalo tayari lina idadi ya watu kwa asilimia 171, taarifa hiyo ilisema.

Wiki iliyopita, nchi jirani ya Afrika Kusini ilieleza wasiwasi kwa Eswatini kukubali wahalifu waliopatikana na hatia, ikisema ina hofu kuhusu wafungwa hao na uwezekano wa "matokeo ya hatari" kwa usalama wa taifa lao.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us