Kwa mujibu wa Ofisi ya Mawasiliano ya Rais wa Uturuki, Erdogan alizungumza kwa njia ya simu na Katibu Mkuu wa NATO, Mark Rutte, kufuatia ombi la Rutte.
Viongozi hao walijadili maendeleo ya hivi karibuni ya vita kati ya Urusi na Ukraine, pamoja na masuala ya kikanda na ya kimataifa.
Erdogan alieleza kuwa hatua zimepigwa katika mazungumzo ya Istanbul yanayolenga usitishaji wa kudumu wa mapigano kati ya Urusi na Ukraine, na akaeleza umuhimu wa kuhakikisha kuwa mchakato huo unaleta manufaa katika masuala ya kibinadamu.
Kwa upande wake, Rutte alitoa maoni yake kuhusu hali ya Ukraine kuelekea mkutano wa Alaska kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Urusi Vladimir Putin. Erdogan alisema kuwa Uturuki inafuatilia kwa karibu mkutano huo unaotarajiwa kufanyika.
Trump na Putin wanatarajiwa kukutana huko Alaska siku ya Ijumaa saa 5:30 asubuhi kwa saa za huko sawa na (1930 GMT).
Huu utakuwa mkutano wa kwanza kati ya marais walioko madarakani wa Marekani na Urusi tangu kuanza kwa vita vya Moscow-Kiev, ambavyo sasa vinaelekea kutimiza miaka mitatu na nusu.