Rais Cyril Ramaphosa amewataka raia wa Afrika Kusini kushirikiana kutafuta suluhu kwa matatizo mengi yanayoyakabili nchi, akizindua mchakato wa "majadiliano ya taifa" siku ya Ijumaa ambao wakosoaji waliushtumu.
Mashauriano ya umma kote nchini kwa taifa la Afrika lenye viwanda vingi zaidi ambalo bado linakabiliwa na umaskini mkubwa na ukosefu wa usawa miaka 30 baada ya kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi.
"Sote tunakubaliana kuwa vitu vingi havifanyi kazi katika nchi yetu," Ramaphosa aliambia mkutano wa watu zaidi ya 1,000 akiweka dira ya mikutano katika maeneo mbali mbali lte nchini katika miezi sita hadi tisa.
"Kwa kuja pamoja, tuzungumze baina yetu, tunaweza kupata suluhu kwa namna ya kuweka mambo mengi sawa hasa yale ambayo hayaendi sawa katika nchi yetu kwa pamoja," alisema.
Mabadiliko ya masuala ya ardhi
Miongoni mwa matatizo ambayo Rais Cyril Ramaphosa ameyataja ni ukosefu wa ajira ambao umepita zaidi ya asilimia 33 na ukosefu wa usawa, ikiwa ni moja ya takwimu mbaya duniani.
Vipaumbele vilivyoorodheshwa na waandaaji ni pamoja na kiwango cha juu cha uhalifu na mabadiliko katika masuala ya ardhi, huku ardhi kubwa ya kilimo ikiwa bado inamilikiwa na wazungu walio wachache.
Chama cha Ramaphosa cha African National Congress (ANC) kinaangazia majadiliano kuwa "mazungumzo baina ya raia wa Afrika Kusini" kuangazia kuhusu mustakabali bora, lakini wakosoaji wameshtumu hatua hiyo.
Chama cha Democratic Alliance, chama cha pili kwa ukubwa katika serikali ya maridhiano ya kitaifa, kimeutaja mchakato huo kama "usio na msingi" na wa "kupoteza’’ pesa na kwamba hakitoshiriki.
Dira ya pamoja
Mkutano huo wa siku mbili ulisusiwa na wanaounga mkono majadiliano, ikiwemo rais wa zamani Thabo Mbeki, baada ya malalamiko kuwa umeharakishwa na wasiwasi kuhusu bajeti.
Ramaphosa aliomba raia kutoka sehemu zote za nchi hiyo ya watu milioni 63 kushiriki.
"Lazima tulenge kukamilisha mchakato huu tukiwa na dira ya pamoja ya taifa: ambayo ni ya ujasiri, kuhamasisha, na iwe inawezekana kuitekeleza," alisema.