Bila shaka utakuwa umetambua. Kuna wanaume na wanawake katika vyombo vikubwa vya habari vya magharibi ambao wanaruhusu watu wenye kauli zenye utata kuzungumza wakati wanapoangazia udhalilishaji wa Gaza, kama kwamba huko ni vita kati ya majeshi ya mataifa mawili.
Tunachoshuhudia ni dhulma katika sehemu — ambayo wakati mmoja ilitajwa kuwa gereza la wazi na kambi ya mauaji — bila shaka siyo vita lakini janga kubwa sana kwa watu katika karne ya 21.
Hatuna haja ya kueleza madhila wanayopitia watu milioni 2.3.
Tunajua kuhusu mateso haya tayari. Tumesoma kuyahusu. Tumetazama wanayopitia. Na yametushtusha sana.
Dunia mbili
Ile sehemu tunayoiita Gaza leo imeharibiwa sana, ambapo Wapalestina walio njaa aidha wamekufa au hawajulikani kama wako hai. Wao na watoto wao wanaelezwa kuwa "wafu wanaotembea."
Katika vituo vya kusambazwa vyakula wanajeshi wa Israel wanawaua watu kila siku, na utu wao umedunishwa kiasi cha mtu kuwa tayari kufa kwa ajili ya kiroba cha mchele, pakiti ya maziwa, dumu la maji.
Ilhali, kilomita chache kutoka hapo, upande wa pili wa mpaka, maduka yamejaa vyakula na watu wanaendelea na maisha yao. Wakitembea mitaani. Wanakunywa kahawa yao. Wakitizama filamu zao. Kusoma vitabu vyao vya Torah. Kwenda kwa daktari wa meno. Kuwakumbatia watoto wao. Kusikiliza mziki na kufanya mapenzi.
Kwa hakika, hii ni mitizamo miwili tofauti.
Maswali mengi kwetu.
Kuna uhalali gani wa kuwanyima watoto chakula? Kuna haki gani ya kuendeleza unyama huo mara kwa mara?
Na nini kinachowafanya raia wa Israel kuungwa mkono harakati za kibaguzi za wanasiasa na jeshi lao?
Waandishi, kama watu wengine, wangekuwa salama iwapo wasingeshiriki katika mijadala kama hiyo.
Dunia isiyojali
Kitu kimoja kiko wazi. Gaza inaungua. Kwa hiyo, kwa nini dunia haijawashurutisha wale wenye uwezo kuingilia kati na kumaliza mauaji ya halaiki Gaza?
Kwa kifupi: Marekani, inayojisifu kuwa “kiongozi wa dunia huru”, bado inasisitiza kuunga mkono Israel.
Kiasi kwamba, imekuwa mara kwa mara ikipiga kura ya turufu kukandamiza juhudi zozote za wajumbe wengine wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kumaliza vurugu hizo eneo la Gaza.
Na serikali zingine katika mataifa ya Magharibi zimeamua kutazama tu.
Ukweli, ukimya wa ulimwengu wa Magharibi yamefanya kuwe na wasiwasi kuhusu msimamo juu ya madhila ya Gaza na hasa misingi wanayoifuata ya uhuru wa Magharibi, kuonesha kama siyo wakweli.
Lakini watu wengi katika mataifa hayo hayo wamekuwa na msimamo dhidi ya serikali zao, kwa kuona kuwa si jambo tu la kimaadili bali njia ya kuzungumza ukweli.
Sauti zao zimepaa, kwa nguvu, uwazi, na kwa matokeo, hata Marekani, ambayo kwa kawaida kuunga mkono Israel hakuhojiwi. Bila shaka, dalili za mabadiliko ziko kila mahali.
Naam, watoto zaidi ya 18,500 wameuawa kufikia sasa na Israel huko Gaza.
Na kwa sisi Wapalestina, ambao kwa majaaliwa tuko hapa,"tunakula, tunalala vizuri na mitaa yetu inalindwa dhidi ya uhalifu kila siku, kile kinachofanyika "kule", katika ardhi ile ni moto, kitabaki sehemu ya utambulisho wetu, chale ambayo haifutiki.
Na vitabu vyetu vya historia vitasema kuwa hakuna mtoto ambaye alichinjwa Gaza atasahauliwa, hakuna unyama ambao umetekelezwa huko utasahauliwa.
Amezaliwa Haifa 1940, mwandishi, Fawaz Tourki alikimbilia Lebanon na familia yake kufuatia Nakba 1948. Sasa hivi ni mwandishi wa Kipalestina na Marekani, mhadhiri mwenye makazi yake Washington, DC. Miongoni mwa vitabu vyake ni The Disinherited: Journey of Palestinian Exile (1972), Soul in Exile (New York, 1988) na Exile’s Return: The Making of a Palestinian-American (New York, 1995).
Kanusho: Maoni haya ya mwandishi hayaakisi maoni, mitazamo na sera ya uhariri ya TRT Afrika.