AFRIKA
2 dk kusoma
Jeshi la Nigeria laua zaidi ya 'wapiganaji' 100 katika mashambulizi ya angani,ardhini
Kulingana na taarifa, mashambulizi hayo ya kijeshi yanaweza kuwa ni kujibu uvamizi wa wapiganaji wa mara kwa mara, hasa utekaji mwezi uliopita.
Jeshi la Nigeria laua zaidi ya 'wapiganaji' 100 katika mashambulizi ya angani,ardhini
Jeshi la Nigeria laua 'wapiganaji’ zaidi ya 100. / Wengine
tokea masaa 12

Jeshi la Nigeria limewaua wapiganaji zaidi ya 100 wa genge la wahalifu katika mashambulizi ya angani na ardhini mwishoni mwa wiki, kulingana na taarifa za Umoja wa Mataifa zilizoonekana na shirika la AFP Jumatatu.

Makundi haya ya wapiganaji yamekuwa yakishambulia wakazi kaskazini magharibi na katikati mwa Nigeria,kuvamia vijiji, kuteka wakazi kwa kutaka kulipwa kikombozi na kuchoma nyumba baada ya kupora.

Mashambulizi haya ya kijeshi katika eneo lenye mapigano jimbo la kaskazini magharibi la Zamfara yalifanyika usiku wa manane Jumapili katika eneo la Bukkuyum, ambapo ndege za kivita kwa ushirikiano na vikosi vya ardhini ziliwashambulia wapiganaji zaidi ya 400 waliokuwa wamekusanyika katika kambi ya msitu wa Makakkari.

Mashambulizi haya ya kijeshi "huenda ikawa ni majibu ya uvamizi wa mara kwa mara wa wapiganaji, hasa utekaji nyara, katika jimbo hilo mwezi uliopita," taarifa hiyo inasema, ikionesha uhusiano na kupungua kwa harakati za kijeshi hivi karibuni katika jimbo hilo na mashambulizi kadhaa ya wapiganaji.

Siku ya Ijumaa kijiji cha Bukkuyum Adabka kulikuwa na mashambulizi ya wapiganaji na watu kadhaa walitekwa na maafisa wa usalama 13 kuuawa.

Vurugu kuenea

Tatizo hili nchini Nigeria limetokana na mapigano juu ya haki za kutumia ardhi na vyanzo vya maji kati ya wafugaji na wakulima, lakini limechukuwa mkondo mwingine na kuwa uhalifu, huku magenge yakilenga jamii za vijijini ambazo hazijakuwa karibu na ulinzi wa serikali kwa muda mrefu.

Wizi wa mifugo na utekaji nyara ni njia kubwa ya kutafuta pesa katika eneo lenye umaskini la vijijini.

Makundi pia yanatoza wakulima na wachimbaji madini wadogo wadogo kodi.

Mapigano yanasababisha tatizo kubwa na utapiamlo kaskazini magharibi huku mashambulizi yakifanya watu wakimbie mashamba yao.

Licha ya jeshi kupelekwa huko kupigana na makundi ya uhalifu tangu 2015, vurugu zimezidi.

Mwezi Julai, wanajeshi wa Nigeria waliwaua watu 95 wa magenge yenye silaha katika ufyatulianaji wa risasi na ya angani katika jimbo la kaskazini magharibi la Niger.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us