Jamii ya Maasai nchini Kenya pamoja na watetezi wa Mazingira wanedelea kuzua utata dhidi ya kuwepo kwa hoteli ndani ya shamba ya hifadhi ya Maasai mara .
Kampuni ya kimataifa ya hoteli ya Marriott International inatazamia kuanzisha hoteli yake ya kifahari ya The Ritz-Carlton barani Afrika kwenye hifadhi ya Maasai Mara.
Dk. Meitamei Ole Dapash anapinga ujenzi wa Kambi ya Safari ya Ritz-Carlton Sand River kwa misingi kwamba iko kwenye korido ya uhamiaji wa wanyamapori.
Katika barua ya kwanza ya Julai 24, 2025, Dkt.Ole Dapash, Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu, Utafiti na Uhifadhi wa Maasai (MERC), anasema mradi huu unaharibu hifadhi ya asilia.
Tumepata mwasiliano kutoka kwa hoteli hiyo , licha ya wao kuelezea wa nini wamejenga kwa eneo hilo lakini wamekubali kuwa maoni ya wanachi lazima yasikilizwa na maswala ya mazingira yazingatiwe,” Dkt. Dopash amesema.
“ Hakuna kiwango cha sababu ziwe kibiashara au kisiasa ambacho kinafanya uharibifu wa barabara ya wanyama hawa kuwa ya haki,” ameongezea.
Dkt. Mamo B. Mamo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mazingira (NEMA) ilithibitisha mamlaka ya mazingira iliidhinisha mradi huo tarehe 14 Mei 2024.
"Ukaguzi wa Wakaguzi wa Mazingira kutoka kwa Mamlaka mnamo tarehe 31 Julai 2025 ulithibitisha ufuasi wa kituo kwa leseni ya EIA na masharti yaliyomo," Dkt. Mamo alisema katika barua ya tarehe 6 Agosti.
Kambi ya Safari ya Ritz-Carlton Maasai Mara, iliyoko katika Kaunti ya Narok karibu na mpaka na Tanzania, inatazamiwa kufunguliwa rasmi Agosti 15 katika hafla itakayoongozwa na Gavana wa Kaunti ya Narok Patrick Ole Ntutu.
"Tovuti hii inatambulika kimataifa kuwa mojawapo ya njia muhimu zaidi za uhamiaji wa wanyamapori Duniani, na umuhimu wake wa kiikolojia na kiutamaduni hauwezi kubadilishwa. Mimi binafsi nimefanya utafiti kwa eneo hili muhimu kwa miongo kadhaa... eneo hili lilikuwa makazi ya vifaru weusi walio hatarini kutoweka na makundi makubwa ya nyati," alibainisha R. Dapash.
Kambi hiyo itakuwa na vyumba 20 vya mahema, madaraja 2, mgahawa, na vifaa vingine kwenye kipande cha ardhi cha ekari 49.4 kilicho kwenye kingo za Mto .
Katika hoteli hii ya kifahari inaripotiwa kuwa kila mtu atalipa Dola za Marekani 3,500 kwa usiku mmoja, ikiwaahidi wageni fursa ya "kuungana na urembo usiofugwa wa Mto Sand ambapo wanyamapori hukusanyika wakati wa Uhamiaji Mkuu" na pia fursa ya kufurahia moja kwa moja Mpaka wa Kenya-Tanzania ambalo linaunganisha mazingira ya Maasai Mara na Serengeti.