AFRIKA
2 dk kusoma
Maafisa waliofariki katika ajali ya helikopta Ghana wazikwa
Waziri wa Mazingira, Sayansi na Teknolojia Ibrahim Murtala Muhammed na Naibu Mratibu wa Usalama Limuna Muniru Mohammed walizikwa siku ya Jumapili.
Maafisa waliofariki katika ajali ya helikopta Ghana wazikwa
Mazishi ya taifa yaliongozwa na Rais John Mahama./ Wengine
tokea masaa 4

Mamlaka nchini Ghana zimefanikiwa “kutambua vyema” miili minane ya maafisa wa serikali waliofariki katika ajali ya helikopta ya jeshi siku ya Jumatano na kufanya mazishi ya watwili wao.

Mazishi ya Waziri wa Mazingira, Sayansi na Teknolojia Ibrahim Murtala Muhammed na Naibiu Mratibu wa Usalama Limuna Muniru Mohammed, yalifanyika siku ya Jumapili, Agosti 10, Shirika la Habari la Ghana liliripoti.

Mazishi hayo ya kitaifa yaliyoongozwa na Rais John Mahama yalifanyika Ikulu mjini Accra na viongozi wengine walihudhuria ikiwemo Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio na Mwenyekiti wa ECOWAS kwa viongozi wa Nchi na Serikali.

"Kwa hiyo tubadilishe huzuni hiyo na kuwa kichocheo cha kuchukua hatua. Tuwaenzi, sito kwa kutoa machozi, lakini kwa kukumbuka waliyoyafanya wakiwa hai na kile amacho wamekufia … Walitumikia Ghana kwa moyo wao wote, na ni jukumu letu kuendeleza huduma hiyo," Mahama alisema wakati wa hafla hiyo.

Mkewe Rais, Lordina Mahama, pia alihudhuria pamoja na Rais wa zamani John Agyekum Kufuor na Makamu wa Rais wa zamani Dkt Mahamudu Bawumia.

Ajali hiyo ya helikopta ilihusisaha helikopta ya Jeshi la Ghanas Z-9, ambayo ilipotea kwenye rada wakati ikipaaa kutoka Accra Agosti 6, 2025, na kuanguka katika eneo la Adansi-Akrofuom kanda ya Ashanti.

Mamlaka zinasema mashauriano yanaendelea na familia kujadili siku ya mazishi kwa waliobaki, akiwemo Waziri wa Ulinzi Edward Omane Boamah.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us