ULIMWENGU
3 dk kusoma
Mashambulizi dhidi ya Waislamu Uingereza hayaangaziwi na vyombo vya habari
Kwa nini Uingereza inachukulia njama za mrengo wa kulia dhidi ya waislamu, kama uhalifu,na siyo ugaidi? ukimya kwa vurugu dhidi ya Uislamu inaonesha undumakuwili wa vyombo vya habari vya Uingereza na siasa, na kuwepo hatari ya kuruhusu udhalilishaji.
Mashambulizi dhidi ya Waislamu Uingereza hayaangaziwi na vyombo vya habari
Mashambulizi dhdi ya Wasilamu Uingereza yanafumbiwa macho, na kuiweka jamii hiyo kwenye hatari. / AP
1 Septemba 2025

Mapema mwaka huu, katika mji mdogo wa Scotland wa Greenock, mvulana wa umri wa miaka 17, aliyekuwa na itikadi za Hitler, alipanga njama ya kuchoma moto kituo cha Waislamu cha Inverclyde, kuwafungia waumini kwa nje, na kuweka ukatili huo mubashara.

Akiwa amefuata itikadi kali ya mrengo wa kulia ya Anders Breivik na alianza kutumia TikTok akiwa na umri wa 13, aliingia msikitini akijifanya anataka kuingia katika dini ya Uislamu. Alipokamatwa, alipatikana na mabomu ya machozi, bastola, na vifaa vya kuanzisha moto. Pia alikuwa ameandika ilani.

Taarifa hii ni hatari, ila kinachoshtua zaidi ni namna gani taarifa hii haijaangaziwa katika vyombo vya habari Uingereza. Sky News iliripoti, ikiwemo walioshuhudia ikiwemo viongozi wa msikiti , lakini vyombo vingine vyote havikuwa na taarifa ya maana.

Sasa tafakari kama aliyefanya hivyo angekuwa Muislamu, na akapanga njama ya kuwadhuru wanaoabudu ndani ya kanisa au sinagogi. Vyombo vyote vya habari vingetangaza kuwa ni ugaidi. Wanasiasa wangetoa taarifa za kulaani ugaidi.  

Idadi ya watu ni dhahiri

Hii siyo simulizi tu.

Pamoja na kuongezeka kwa mashambulizi, Waislamu bado hawapati ulinzi wa kutosha. Iman Atta, mkurugenzi wa shirika la MAMA anasema kuwa mwaka 2024 mashambulizi yaliongezeka kwa asilimia
73 percent in 2024, huku kukiwa na matukio 5,837 yaliyothibitishwa, ikiwa ishara ya kipindi hatari zaidi kwa Waislamu Uingereza. 

Katika maeneo kama Inverclyde, Waislamu wamelazimika kufanya mipango yao wenyewe ya ulinzi, kufuatilia tabia za watu, na kuwa makini kuhusu hofu ya watu kujificha miongoni mwao.

Pamoja na hayo kuwa mzigo zaidi, inaondoa uaminifu. Waumini wanakuwa na wasiwasi kwamba mtu anayeswali pembeni mwao huenda akawa na nia mbaya. Hilo ni suala linalowaumizi kisaikolojia kwa jamii ambayo tayari imetengwa

Mwezi Februari 2025, serikali ilianzisha kikosi kazi cha kubaini maana halisi kitaifa ya chuki dhidi ya Waislamu.

Kwa Waislamu wengi, ishara hizi za kutatanisha zinaonesha tatizo kubwa zaidi: Chuki dhidi ya Uislamu inatambulika lakini haishughulikiwi kama inavyotarajiwa.

Shirika la misaada la Tell MAMA na IRU wanaendelea kuziba pengo hilo, wakiorodhesha dhulma, kutoa msaada wa kisheria, na kutaka kutambuliwa, lakini wanafanya hivyo hukus serikali na vyombo vya habari vikiwa havioneshi ushirikiano.

Kuwapa nguvu wanaohusika na uhalifu

Kwa kudharau vurugu za chuki kwa Waislamu Uingereza inaingia katika hatari ya kufanya ya Waislamu kuonekana hayana thamani. Ukimya huu unawapa nguvu wanaohusika na uhalifu. Ishara kuwa wenye itikadi kali kuwa wanaweza kufanya wanachotaka bila kukamatwa, na ujumbe kwa Waislamu kuwa usalama siyo suala linalopewa kipaumbele na taifa.

Vyombo vya habari vya Uingereza vinatakiwa kuripoti kuhusu chuki dhidi ya Waislamu kwa uthubutu sawa kama wanavyotoa taarifa za matukio mengine ya kigaidi. Mashambulizi kwa miskiti na jamii yanafaa kuwa zaidi ya kutajwa tu.

Na serikali lazima ijumuishe chuki dhidi ya Waislamu katika mikakati yake ya uhalifu wa chuki na kukabiliana na ugaidi, kuhakikisha kuwa ugaidi wa siasa za mrengo wa kulia unachukuliwa kwa uzito sawa na vitisho vingine vya ugaidi.

Hatimaye, umma lazima wataka watu kuwajibishwa. Uingerea haiwezi kuendelea kufumbia macho taarifa hizi kwa sababu tu walioshambuliwa ni Waislamu. Kama nchi haiwezi kufkiria kufanya chuki dhidi ya Waislamu kuwa suala la dharura, kuna hatari ya kuwepo kwa tatizo kubwa zaidi ambalo halitoweza kufumbiwa macho tena.

CHANZO:TRT World and Agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us