AFRIKA
2 dk kusoma
Hemetti wa RSF aapishwa kama kiongozi wa serikali sanjari huku raia wakiuawa Kordofan
Jeshi la Sudan linasema watu watano kutoka familia moja, ikiwemo wasichana wawili wadogo, waliuawa kwa shambulio la RSF la ndege zisizo na rubani Kaskazini mwa Jimbo la Kordofan kusini mwa Sudan.
Hemetti wa RSF aapishwa kama kiongozi wa serikali sanjari huku raia wakiuawa Kordofan
Familia zilokimbia makazi yao Sudan zikipata hifadhi katika uwanja wa mpira baada ya mashambulizi ya RSF Kordofan, Mei 27, 2025. (Mercy Corps/AP)
30 Agosti 2025

Mohamed Hamdan Dagalo, kiongozi wa vikosi vya wapiganaji vya Rapid Support Forces, ameapishwa kama kiongozi wa serikali sanjari ya Sudan, serikali imesema katika taarifa, kuelekeza nchi katika hatari ya kugawanyika.

Dagalo, anayejulikana kama Hemetti, hajaonekana sana Sudan tangu kuanza kwa vita vya miezi 28 na jeshi la taifa la nchi hiyo, lakini aliapishwa katika mji wa Sudan wa Nyala, taarifa ilisema. Shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha sehemu hasa aliyokuwepo.

Moja ya miji mikubwa ya Sudan, katika eneo la Darfur, Nyala imekuwa kama makao makuu ya RSF, na serikali hiyo imeteua waziri mkuu na baraza la rais, linaloongozwa na Dagalo.

Mji huo ulilengwa na ndege zisizo na rubani siku ya Jumamosi.

Jeshi la Sudan linasema raia watano kutoka kwa familia moja, ikiwemo wasichana wawili wadogo, waliuawa kwa shambulio la RSF la ndege zisizo na rubani Kaskazini mwa Jimbo la Kordofan kusini mwa Sudan.

Mashambulizi hayo ya usiku yalilenga kijiji cha Awlad Al-Sharif katika eneo la Indraba, jeshi lilisema katika taarifa. Wanavijiji wengine sita walijeruhiwa.

Jeshi lilieleza shambulizi hilo kuwa sehemu ya kile walichokiita “muendelezo wa unyama dhidi ya raia na uhalifu wa kivita.” wa RSF

Mashambulizi mabaya

Pamoja na kuwa RSF inadhibiti sehemu kubwa ya Darfur, imekuwa ikipigana vikali na jeshi kwa lengo la kutaka udhibiti wa mji wa Al Fasher, makao makuu ya kihistoria ya eneo hilo.

Maelfu ya raia wamekwama katika sehemu hiyo kwa siku zaidi ya 500, kuwalazimisha kula chakula cha mifugo ili waweze kuishi.

Shirika la UNICEF limesema mapewa wiki hii zaidi ya watoto 1,000 wameuawa kwa mashambulizi ya angani, makombora, na ardhini.

Shirika la Yale Humanitarian Lab limesema Ijumaa kuwa picha za satelaiti zinaonesha kuwa wapiganaji hao wameweka vizuizi, kuzuia watu wasiondoke eneo hilo. Wale waliofanikiwa kuondoka wanaeleza kuwepo kwa mashambulizi mabaya na ujambazi unaotekelezwa na wanajeshi wa RSF.

Jeshi la Sudan limechukuwa udhibiti wa maeneo ya kati na mashariki mwa Sudan, na kuunda serikali tangu kuanza kwa vita, ambapo ilifanya mkutano wake wa kwanza wa baraza la mawaziri mapema wiki hii.

Kanda hiyo yenye ukubwa ya Kordofan iko katikati ya ngome ya pande zote mbili zinazozozana na bado kuna mapigano na mashambulizi katika vijiji vidogo.

Vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe vimesababisha njaa kubwa kwa nusu ya raia wa Sudan, uchumi ulioporomoka, na kusababbisha hali mbaya zaidi kwa watu duniani.

CHANZO:TRT World
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us