AFRIKA
1 dk kusoma
Shirika la Kenya Airways lapata hasara ya dola milioni 93
Shirika la ndege la Kenya Airways limepata hasara kipindi cha nusu ya kwanza ya 2025. Kampuni hiyo imepata hasara ya dola milioni 93 baada ya kodi, ikiwa ni tofauti kubwa na faida ya dola milioni 4 waliopata katika kipindi kama hicho 2024.
Shirika la Kenya Airways lapata hasara ya dola milioni 93
Ndege za Shirika la Kenya Airways. / Picha: Reuters
27 Agosti 2025

Idadi ya abiria wa shirika la Kenya Airways ilipungua kwa asilimia 14 hadi milioni 2.2. Kushuka huku kunasemekana ni kutokana na ndege tatu za Boeing 787-8 za Dreamliner kutofanya kazi kwa ajili ya kufanyia ukarabati, jambo ambalo lilipunguza uwezo wa shirika na ufanisi.

Afisa Mtendaji Mkuu Allan Kilavuka anasema ndege moja ya Dreamliner ilirudi kuanza tena kufanya kazi mwezi Julai, na nyingine zinatarajiwa kuanza tena kazi 2026.

Katika kuimarisha nafasi yake, Kenya Airways inajipanga kutafuta mtaji mwingine wa zaidi ya fedha zaidi ya dola milioni 500 na watahitaji kupata idhini kutoka kwa wenye hisa kwa mpango huo.

Matatizo ya shirika hilo yanakuja miezi kadhaa baada ya kupata faida nzuri ya mwaka mzima katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja mwaka 2024, walipopata faida ya karibu dola milioni 40.

CHANZO:TRT Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us