Wizara ya Afya ya Sudan ilitangaza Jumanne kwamba ilirekodi maambukizi mapya ya kipindupindu 1,210, pamoja na vifo 36, ndani ya wiki moja.
Katika taarifa yake, wizara hiyo ilisema maambukizi hayo mapya yalifikisha jumla ya maambukizi ya kipindupindu kufikia 102,831, ikijumuisha vifo 2,561 tangu kuzuka kwake Agosti 2024, hata hivyo yalipungua katika baadhi ya majimbo na kuongezeka kwa mengine, bila kutaja ni yapi, taarifa iliongeza.
Mnamo Agosti 6, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilithibitisha maambukizi ya kipindupindu katika majimbo yote 18 ya Sudan.
Maafa ya kiafya nchini Sudan yanakuja wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya jeshi na vikosi vya RSF vilivyoanza tangu Aprili 2023.
Mzozo huo umesababisha makumi ya maelfu ya watu kupoteza maisha na mamilioni ya wengine kuyahama makazi yao.
