Kwa mujibu wa vyanzo vya kidiplomasia vya Uturuki, Hakan Fidan na Marco Rubio wamejadili mchakato unaoendelea wa amani ili kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine, pamoja na hali ya hivi karibuni katika Ukanda wa Gaza.
Wakati wa mazungumzo yao ya simu siku ya Alhamisi, Fidan alieleza kuwa Ankara iko tayari kutekeleza wajibu wake katika mchakato wa amani kati ya Moscow na Kiev.
Mapema leo, marais wa Uturuki na Ukraine pia walijadili mchakato wa amani kati ya Ukraine na Urusi.
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, alimfahamisha mwenzake wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, kuwa Uturuki inaendelea na juhudi zake kuhakikisha kuwa vita vinaisha kwa amani ya kudumu.
Katika mazungumzo hayo yaliyogusia pia hali ya sasa huko Gaza, Fidan alisisitiza hitaji la dharura la kuboresha hali ya kibinadamu katika eneo hilo.
Waziri hao wawili pia walijadili hali nchini Syria pamoja na mahusiano ya mataifa mawili.