AFRIKA
1 dk kusoma
Mzimu wa Shakahola wazuka tena Kenya, miili 32 imefukuliwa
Miili 32 imefukuliwa wiki hii katika kijiji cha Kwa Binzaro, karibu na Shakahola, Kaunti ya Kilifi nchini Kenya.
Mzimu wa Shakahola wazuka tena Kenya, miili 32 imefukuliwa
Shughuli za utafutaji zinaendelea huku watu 11 wakikamatwa hadi sasa. / / Reuters
tokea masaa 9

Mauaji hayo yanahusishwa na imani potofu ya kufunga hadi kufa inayohusishwa na mhubiri Paul Mackenzie wa kanisa la Good News International.

Dkt. Richard Njoroge, daktari wa serikali anayesimamia uchunguzi huo, amesema zoezi la ufukuaji limeanza wiki iliyopita na hadi sasa jumla ya miili 32 imepatikana.

Tukio hili linafufua maumivu ya vifo vya Shakahola mwaka 2023, ambapo watu zaidi ya 400 walifariki kwa njaa wakifuata mafundisho ya “mwisho wa dunia.”

Shughuli za utafutaji zinaendelea huku watu 11 wakikamatwa hadi sasa.

Serikali ya Kenya imeahidi msako mkali na udhibiti zaidi kwa madhehebu hatari yanayohusiana na imani potofu kama hii.

CHANZO:Reuters
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us