Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uturuki Super League Galatasaray wamekamilisha mchakato wa kumsaini winga wa Bayern Munich Leroy Sane, kwa kile wengi wanakitaja kuwa hatua muhimu kwa soka la Uturuki.
Raia huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 29 aliwasili Istanbul 12 Juni, na kupokelewa na idadi kubwa ya mashabiki pamoja na wengine kufuatilia mitandaoni.
Mashabiki zaidi ya milioni 1 walijiunga kwa matangazo mubashara ya kuwasili kwa ndege yake katika mtandao wa YouTube wa Galatasaray. Klabu hiyo pia ilionesha picha za Sane akiwa katika uwanja wa ndege wa Istanbul akiwa amevaa kitambaa chao maarufu na kutangaza kuwa wameanza mazungumzo rasmi.
Kulingana na vyombo vya habari vya Uturuki, Sane ametia saini mkataba wa miaka mitatu akipata mshahara wa dola milioni 11.5 kwa mwaka. Anajiunga na klabu hiyo ya Istanbul baada ya mkataba wake na Bayern kumalizika mwishoni mwa mwezi huu.
Klabu hiyo ilianzishwa 1905 na wanafunzi wa shule ya upili ya kifahari ya Istanbul Galatasaray.
Imeshinda mataji 25 ya Ligi Kuu ya Uturuki, na kuifanya kuwa timu yenye mafanikio makubwa zaidi katika Ligi Kuu. Mafanikio yao makubwa zaidi ni waliposhinda Kombe la UEFA na kombe la Super Cup la UEFA 2000.
Katika miaka iliyopita, klabu hiyo imekuwa na wachezaji nyota kama vile Gheorghe Hagi, Didier Drogba, Wesley Sneijder, Claudio Taffarel, na Fernando Muslera, ambao wote wameacha alama kubwa kwenye klabu hiyo.
Uhamisho wa mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani Leroy Sane kuja Galatasaray huenda ikawa hatua muhimu zaidi kwa soka la Uturuki, anasema mchambuzi wa michezo Nedim Yigit, ambaye anaamini kuwa uhamisho huu ni ishara ya ubora na ari kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu.
“Sane anajulikana kote duniani, aligunduliwa na Norbert Elgert akiwa Schalke na akawa zawadi kwa soka la Ujerumani,” Yigit ameiambia TRT World.
Sane alianza kucheza soka akiwa na klabu ya Schalke kabla kuelekea Manchester City, ambapo alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu ya England chini ya Kocha Pep Guardiola. Alienda Bayern Munich 2020, na kucheza katika klabu hiyo mara 220, pamoja na kufunga magoli 61 na kutoa msaada wa magoli mara isiopungua 55.
Yigit anasema kuwa na mchezaji mwenye sifa ya kimataifa kutaimarisha nafasi ya Galatasaray na hadhi ya ligi duniani, kutoka kwa wafadhili na mauzo ya jezi.
“Tayari Galatasaray imefanikiwa kuliona hili kutoka kwa wachezaji kama Icardi na Osimhen. Sane anaweza pia kufungua njia ya kuwaleta wachezaji wakubwa zaidi kwenye klabu hiyo.”
Mbali na kuwa na matokeo mazuri nyumbani, Yigit anaamini uhamisho huo unaonesha ari ya Galatasaray ya kuimarika barani Ulaya, hasa katika michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya.
Kuwa na wachezaji kama raia wa Nigeria Victor Osimhen, Wajerumani Marc-Andre ter Stegen na Ilkay Gundogan pamoja na Mreno Bernardo Silva — wanaosemekana kuwa karibu kutia saini zao — pia wataleta matumaini zaidi.
“Kile ambacho wakati mmoja kilionekana kama kisichowezekana sasa ni jambo la kawaida,” aliongeza.
Kuhusu umahiri wa Sane uwanjani, Yigit anasema mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani anatarajiwa kuwa mshambuliaji hatari. “
Mashabiki
Kuna furaha kubwa miongoni mwa mashabiki. Wakieleza furaha yao kwa TRT World, Mustafa Aslan, shabiki wa Galatasaray, anasema, “Leroy Sane anajulikana kwa mbio zake, mbinu za uwanjani, na namna ya kuzuia mpira.”
“Uhamisho kama huu kwa ligi ya Uturuki barani Ulaya. Tukiwa na mchezaji nyota kama Sane upande wetu, nadhani tunaweza kukabiliana na timu kubwa barani Ulaya,” ameongeza.
Shabiki mwingine, Omer Arikan, amefurahishwa na hilo lakini anaomba kuwe na mizania.
“Hizi ni habari njema, lakini tusiwasahau wachezaji wa nyumbani. Wachezaji wasiopungua wawili wa Uturuki muhimu wawepo kwenye kikosi cha kwanza cha watu kumi na moja. Kuwepo kwa wachezaji wa nyumbani ni muhimu.”
Abdullah Tarik, pia kutoka Istanbul, anasema amefurahishwa sana,
“Sane anakuja akiwa na miaka 29 ni jambo zuri sana kwa soka la Uturuki. Galatasaray imefanya kisichowezekana kwa wachezaji kama hawa. Mwaka uliopita, ilikuwa Osimhen. Wanasaidia soka la Uturuki kuimarika na kufanya watu waangazie ligi hiyo.”
Busra Sancar, shabiki wa muda mrefu wa Galatasaray, anaeleza umuhimu wa uhamisho huu.
“Kuwa na wachezaji bora wa dunia kama Sane kwenye ligi yetu kunatoa fursa kwa wachezaji wadogo wa Uturuki kumuangazia mtu ambaye atakuwa mfano mzuri kwao. Ana nidhamu, anaweza kucheza kwa ubora, na ni mbunifu.”
Iwapo kutuwa kwa Sane itakuwa mwanzo wa enzi mpya kwa soka la Uturuki itafahamika baada ya mchezaji kuonekana uwanjani - lakini kuna matumaini tayari kote katika Ligi Kuu ya Uturuki Super League.