UTURUKI
2 dk kusoma
Bunge la Uturuki lataka uanachama wa Israel kusitishwa katika UN kutokana na mashambulizi ya Gaza
Israel imeua takriban Wapalestina 63,000 huko Gaza tangu Oktoba 2023. Vita hivyo vimeharibu eneo hilo, ambalo sasa linakabiliwa na njaa kali.
Bunge la Uturuki lataka uanachama wa Israel kusitishwa katika UN kutokana na mashambulizi ya Gaza
Azimio hilo pia limetoa wito kwa mabunge yote ya kitaifa kukata uhusiano wa kijeshi na kibiashara na Israel. / / AA
tokea masaa 7

Bunge la Uturuki limepitisha azimio kali likilaani uvamizi ulioongezeka wa Israel katika Ukanda wa Gaza na kuituhumu kwa kutekeleza mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina.

Katika azimio hilo, Bunge limetangaza ya kwamba: "Tunatoa wito wa kusitishwa kwa uanachama wa Israel katika Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine za kimataifa hadi itakapoacha sera zake za mauaji ya halaiki."

Azimio hilo pia limezitaka mabunge yote ya kitaifa duniani kuvunja uhusiano wa kijeshi na kibiashara na Israel, na kuchukua hatua za kuondoa vikwazo dhidi ya Palestina.

Azimio hilo lilitolewa mwishoni mwa kikao maalum cha Bunge kilichoitishwa kwa ajili ya kujadili hali ya Gaza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, alihutubia kikao hicho na kutoa taarifa kwa wabunge kuhusu janga la kibinadamu linaloendelea Gaza.

Aliituhumu Israel kwa kutenda uhalifu ambao aliueleza kuwa miongoni mwa "nyakati za giza kabisa katika historia ya binadamu."

“Israel kwa miaka miwili imekuwa ikitenda uhalifu wa mauaji ya halaiki huko Gaza, ikidharau kabisa maadili ya msingi ya kibinadamu mbele ya macho ya dunia,” alisema Fidan.

Mnamo Novemba iliyopita, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilitoa hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Waziri wake wa zamani wa Ulinzi Yoav Gallant kwa tuhuma za uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu huko Gaza.

Pia, Israel inakabiliwa na kesi ya mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kutokana na vita vyake dhidi ya Gaza.

CHANZO:TRT World
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us