AFRIKA
3 dk kusoma
Marekani kujadili nafasi ya Kenya kama Mshirika Mkuu asiye mjumbe wa NATO
Kuteuliwa kuliifanya Kenya kuwa na uhusiano wa juu wa ushirikiano wa kiulinzi na Marekani na ina uwezo wa kuunda fursa za muda mrefu za suluhu za ulinzi wa kibiashara wa Marekani.
Marekani kujadili nafasi ya Kenya kama Mshirika Mkuu asiye mjumbe wa NATO
Rais wa Kenya William Ruto alifanya ziara rasmi nchini Marekani May 2024/ picha: Reuters
6 Agosti 2025

Utawala wa Rais wa Marekani, Donald Trump, umependekeza kuhakiki upya nafasi ya Kenya kama Mshirika Mkuu asiye wa NATO, miezi michache tu baada ya Kenya kupewa hadhi ya nchi ya kwanza ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kupata sifa hiyo.

Marekani kutaja nchi kama Mshirika Mkuu asiye wa NATO (MNNA) ni chini ya sheria ya Marekani ambayo huitoa kwa nchi za kigeni kwa ajili ya manufaa maalumu katika maeneo ya ushirikiano wa kibiashara na usalama.

Uteuzi huo, uliotolewa Juni 24, 2024, na aliyekuwa rais wa Marekani Joe Biden uliiweka Kenya katika nafasi ya kuwa mshirika mkuu wa Marekani barani Afrika hivyo kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili katika nyanja za ulinzi, usalama na kiuchumi.

Lakini sasa Seneta wa Marekani James Risch amependekeza marekebisho ya Sheria ya Uidhinishaji wa Kitaifa wa Ulinzi kwa Mwaka wa Fedha wa 2026, ambayo yanalenga kukagua uteuzi wa Kenya ndani ya siku 90.

Tathmini ya seneti itazingatia nini?

Kuteuliwa kuliifanya Kenya kuwa na uhusiano wa juu wa ushirikiano wa kiulinzi na Marekani na ina uwezo wa kuunda fursa za muda mrefu za suluhu za ulinzi wa kibiashara wa Marekani.

Mapendekezo ya seneta Risch ni kutathmini sera za kigeni na za kidiplomasia za Kenya kama vile kujifungamanisha na Marekani na ushirikiano wake na China, Urusi na Iran.

Pia yatakayotahminiwa ni pamoja na makubaliano yanayowezekana ya Kenya, uhusiano wa kisiasa au kifedha na wanamgambo wenye silaha kama vile al-Shabaab na Kikosi cha Rapid Support Forces cha Sudan (RSF).

"Maelezo ya kina kuhusu uhusiano wa kijeshi na usalama wa Serikali ya Kenya na Jamhuri ya Watu wa China, Shirikisho la Urusi, na Iran, ikiwa ni pamoja na mazungumzo yoyote, makubaliano, au shughuli za pamoja tangu Juni 24, 2024," ilisoma sehemu ya tovuti ya Bunge la Marekani.

Nchi za Afrika ambazo zimetambuliwa na Marekani kama Mshirika Mkuu asiye wa NATO ni Misri, Kenya na Morocco na Tunisia.

Nchi nyengine ni Argentina, Australia, Bahrain, Brazil, Colombia, Israel, Japan, Jordan, Kuwait, New Zealand, Pakistan, Philippines, Qatar, Korea Kusini na Thailand.

Manufaa yake

Nchi inaweza kupata mikopo ya nyenzo, vifaa, au vifaa kwa madhumuni ya utafiti wa ushirika, maendeleo, majaribio au tathmini kutoka Marekani.

Inaweza kuchaguliwa kama eneo la Hifadhi ya Vita vinayomilikiwa na Marekani kuwekwa kwenye eneo nje ya vituo vya kijeshi vya Marekani.

Nchi husika inaweza kuingia makubaliano na Marekani kwa ajili ya kupata mafunzo na ina idhini ya kuzingatiwa ili kununua silaha.

Nchi inayopewa heshima hii na Marekani inaweza kufanya makubaliano rasmi na Idara ya Ulinzi ya Marekani kwa madhumuni ya kufanya utafiti wa ushirika na miradi ya maendeleo kuhusu vifaa vya ulinzi na risasi.

Nchi husika inaweza kupata zabuni za matengenezo, ukarabati wa vifaa vya Idara ya Ulinzi ya Marekani nje ya Marekani.

Muwasda wa seneti ya Marekani ukiidhinishwa marekebisho hayo yatahitaji Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio kufanya ukaguzi na kuwasilisha matokeo kwa Kamati husika ndani ya siku 180.


CHANZO:TRT Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us