Kocha wa Uganda, Morley Byekwaso alikiri kwamba timu yake ilikabiliwa na shinikizo ilipoangukia kichapo cha 3-0 kutoka kwa Algeria mbele ya mashabiki wao wa nyumbani katika mechi yao ya ufunguzi ya Kundi C ya TotalEnergies CHAN 2024.
The Cranes walilemewa tangu mwanzo, kwa kuruhusu mabao matatu na kujitahidi kukabiliana na uchezaji mkali wa mashambulizi wa Algeria na muundo mzuri wakati wa mchezo wa Jumatatu.
Kwa Byekwaso, utendaji ulifichua mapungufu katik amaandalizi kiakili na kimkakati.
"Tulikuja kuonyesha ubora wetu, lakini tulishindwa katika safu yetu ya ulinzi na tukalipa gharama," alisema baada ya kipenga cha mwisho.
"Timu ilikuwa na wasiwasi. Hatukuweza kufanya mabadiliko, na presha ilisababisha timu kushindwa."
kikosi cha ulinzi cha Uganda kilisambaratika mapema, huku Ayoub Ghezala akifunga bao la mkwaju.
Mabao mengine kutoka kwa Abderrahmane Meziane na Soufiane Bayazid yalizidisha masaibu ya Cranes. Licha ya hatua chache za matumaini, Uganda ilishindwa kubadilisha nafasi zao au kuendana na nidhamu ya kiufundi ya Algeria.
"Baada ya bao la kwanza, tulivunjika moyo. Tulipoteza nafasi, tukapoteza mechi kirahisi sana, na kushindwa kudhibiti mechi," Byekwaso alikiri.
"Ninaamini tuna wachezaji wazuri. Sasa ni lazima tutulie kimawazo, tukubali makosa yetu, na tufanye kazi kujiimarisha kabla ya mchezo unaofuata."
Uganda wanakabiliwa na mechi ya pili muhimu dhidi ya Guinea siku ya Ijumaa 8/8, huku wakijaribu kuokoa kampeni yao ya CHAN.
Algeria wanashikilia sasa uongozi wa Kundi C kwa alama tatu safi ya mabao matatu.
Katika mechi zote sita walizocheza za CHAN awali, Uganda bado haijafuzu mbele ya hatua ya makundi ya michuano hiyo. Ilitarajiwa pengine kwa kuungwa mkono na mashabiki wa nyumbani, The Uganda Cranes wangeweza kuandika upya historia na kuboresha rekodi yao katika shindano hilo.
Pengine mechi zijazo.