ULIMWENGU
1 dk kusoma
Gwiji wa soka wa Ureno Jorge Costa afariki dunia kwa mshtuko wa moyo
Costa anakumbukwa zaidi kama nahodha wa kikosi cha Fc Porto chini ya kocha Jose Mourinho kilichotwaa ubingwa wa Ulaya mnamo 2004, Porto walipoifunga AS Monaco 3-0 kwenye fainali.
Gwiji wa soka wa Ureno Jorge Costa afariki dunia kwa mshtuko wa moyo
Nahodha za zamani wa Porto, Jorge Costa./Picha:Getty
5 Agosti 2025

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Porto, Jorge Costa amefariki dunia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa siku ya Jumanne na klabu ya Porto, inasema kuwa Costa, mwenye umri wa miaka 53, alifariki dunia kwa mshtuko wa moyo, akiwa ndani ya viunga vya viwanja vya mazoezi vya klabu hiyo.

"Gwiji wa klabu ya Porto na mkurugenzi wetu hatunaye tena,” ilisema taarifa iliyotolewa na klabu hiyo siku ya Jumanne.

Costa anakumbukwa zaidi kama nahodha wa kikosi cha Fc Porto chini ya kocha Jose Mourinho kilichotwaa ubingwa wa Ulaya mnamo 2004, Porto walipoifunga AS Monaco 3-0 kwenye fainali.

Akiwa na Porto, Costa alishinda mataji nane ya Ligi Kuu ya Porto, na Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2004.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us