AFRIKA
1 dk kusoma
Tanzania yavuna alama sita baada ya kuifunga Mauritania
Michuano ya CHAN 2024 inaandaliwa kwa pamoja na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.
Tanzania yavuna alama sita baada ya kuifunga Mauritania
Bao la 'Taifa Stars' lilifungwa katika dakika ya 89 ya mchezo na Shomari Kapombe./Picha:@Tanfootball
tokea masaa 16

Tanzania imezidi kuchanja mbuga kwenye michuano ya CHAN 2024 baada ya kuifunga Mauritania kwa bao 1-0, katika mchezo wao wa pili wa Kundi B, uliofanyika Agosti 6, 2025 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Bao pekee la ‘Taifa Stars’ lilifungwa na Shomari Kapombe aka ‘Baba Esther’ katika dakika ya 89 ya mchezo, na kuipa alama nyingine tatu muhimu kwenye michuano hiyo maalumu kwa wachezaji wanaoshiriki ligi za ndani.

Matokeo hayo yanaifanya Mauritania kubakia na alama moja baada ya suluhu yao ya 0-0 na Madagascar, huku Tanzania ikiongoza kundi hilo, ikiwa na alama sita na magoli matatu, baada ya ushindi wao wa awali dhidi ya Burkina Faso.

Katika mchezo awali, timu ya taifa ya Burkina Faso iliibugiza Jamhuri ya Afrika mabao 4-2, katika mchezo wa Kundi B.

Michuano ya CHAN 2024 inaandaliwa kwa pamoja na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us