AFRIKA
1 dk kusoma
Uganda yazoa alama 3 zingine kwa ushindi dhidi ya Niger
Timu ya Korongo wa Uganda waliwapa cha kufurahia mashabiki wa nyumbani walipoipa kipigo Niger magoli 2-0 katika uwanja wa Taifa wa Mandela.
Uganda yazoa alama 3 zingine kwa ushindi dhidi ya Niger
Timu ya Uganda ikisherehekea ushindi dhidi ya Niger. / @OfficialFUFA
tokea masaa 13

Uganda wana cha kufurahia baada ya kuwa na alama sita kibindoni hii ni baada ya ushindi wao wa Jumatatu dhidi ya Menas wa Niger.

Uganda iligawanya magoli yake katika kila kipindi, ikienda mapumziko wakiwa na goli moja tayari dhidi ya wapinzani wao.

 Allan Okello aliipatia timu hiyo ya nyumbani bao la kwanza katika dakika ya 25, naye Joel Sserunjogi akakamilisha furaha ya mashabiki alipoingiza kimiani goli la pili katika dakika ya 56.

Timu hiyo sasa ina jumla ya alama 6 baada ya kucheza mechi tatu. Mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Algeria walizabwa mabao 3-0, kisha wakalipiza kisasi kwa magoli sawa na hayo dhidi ya Guinea.

Korongo wa Uganda ambao ni wenyeji wenza wako kundi C pamoja na Afrika Kusini na Algeria.

Katika mechi ya awali Jumatatu Afrika Kusini ilipata ushindi wa magoli mawili kwa moja dhidi ya Guinea.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us