AFRIKA
2 dk kusoma
Umoja wa Afrika wahuzunishwa na ajali ya helikopta iliyoua mawaziri wawili wa Ghana
Kupitia taarifa yake, mwenyekiti huyo alituma salamu zake za rambirambi kwa Rais wa Ghana John Dramani Mahama, serikali ya nchi, watu wa Ghana, pamoja na familia za wafiwa, kufuatia ajali hiyo iliyotokea Agosti 6, 2025.
Umoja wa Afrika wahuzunishwa na ajali ya helikopta iliyoua mawaziri wawili wa Ghana
Ajali ya Helikopta yaua mawaziri wawili Ghana./Picha:Wengine
tokea masaa 17

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Mahmoud Ali Youssouf, amesikitishwa na ajali ya helikopta iliyogharimu maisha ya watu 8, wakiwemo mawaziri wawili nchini Ghana.

Katika taarifa yake iliyotolewa Agosti 6, 2025, Youssouf alisema kuwa amesikitishwa na ajali hiyo, ambayo imechukua uhai wa Waziri wa Ulinzi wa Ghana Edward Omane Boamah na mwenzake wa Sayansi na Teknolojia, Ibrahim Murtala Mohammed.

Kupitia taarifa yake, mwenyekiti huyo alituma salamu zake za rambirambi kwa Rais wa Ghana John Dramani Mahama, serikali ya nchi, watu wa Ghana, pamoja na familia za wafiwa, kufuatia ajali hiyo iliyotokea Agosti 6, 2025.

“Umoja wa Afrika upo pamoja na Ghana katika wakati huu mgumu. Roho za marehemu zipumzike kwa amani.”

Ajali hiyo ilitokea mara baada ya helikopta hiyo kuondoka kutoka jijini Accra majira ya saa tatu asubuhi (kwa saa za Afrika Mashariki), ikielekea kwenye mji wa Obuasi kushuhudia tukio la kupambana na uchimbaji haramu wa madini.

Picha mbalimbali za mitandaoni, zilionesha mabaki ya helikopta hiyo ambayo ilikuwa imeungua.

Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo ameamuru bendera zote zipepee nusu mlingoti, kufuatia ajali hiyo.

Wengine waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni pamoja na Mratibu wa taifa wa masuala ya usalama wa Ghana na Waziri wa zamani wa Kilimo wa nchi hiyo Alhaji Muniru Mohammed, pamoja na Makamu Mwenyekiti wa chama tawala Samuel Sarpong.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us