AFRIKA
2 dk kusoma
Magaidi 70 wa al-Shabaab wauawa katika operesheni ya kijeshi Somalia
Wanajeshi wawili wameuawa na wengine 12 kujeruhiwa wakati wa operesheni katika kanda ya Lower Shabelle, Wizara ya Ulinzi imesema
Magaidi 70 wa al-Shabaab wauawa katika operesheni ya kijeshi Somalia
5 Agosti 2025

Magaidi wasiopungua 70 wa al-Shabaab wameuawa katika operesheni ya kijeshi iliyofanywa na jeshi la Somalia likiungwa mkono na vikosi vya amani vya Muungano wa Afrika katika kanda ya Lower Shabelle, Wizara ya Ulinzi imesema Jumatatu.

Wanajeshi wawili wa Somalia (SNA) waliuawa na wengine 12 kujeruhiwa wakati wa mapigano hayo, ilisema katika taarifa.

Wizara imesema jeshi la Somalia na lile la Uganda, yanayoungwa mkono na washirika wa kimataifa wamewakabili vikali al-Shabaab kufuatia “operesheni iliyofanikiwa na iliyopangwa vizuri”

Inaseme operesheni ‘‘Silent Storm” ililenga kambi muhimu katika mji wa Bariire, na kuvunja ulinzi wake.

“Wakati wa operesheni hiyo, al-Shabaab ilijaribu kufanya shambulizi la kujilipua kwa kutumia gari lililojaa vilipuzi. Hata hivyo, wanajeshi walikabiliana kwa ujasiri na ukakamavu, na kufanikiwa kukata makali vilipuzi kwenye magari yote kabla ya kufanya mashambulizi,” taarifa hiyo ilisema.

Taarifa hiyo ya wizara inakuja sikuc chache kabla ya AUSSOM kusema kuwa magaidi zaidi ya 50 wa al-Shabaab waliuawa katika operesheni ya pamoja ya kijeshi na jeshi la Somalia katika sehemu hiyo hiyo.

Bariire ni mji muhimu wa kwa ukulima ulio kilomita 73 (maili 45) kusini magharibi mwa mji mkuu Mogadishu.

Al-Shabaab, ambao wamekuwa wakiendeleza uasi dhidi ya serikali ya Somalia kwa zaidi ya miaka 16, mara nyingi huwa wanalenga maafisa wa usalama, maafisa wa serikali na raia.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us